HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 2, 2019

DCAT YATOA HUDUMA YA AFYA BURE KWA ZAIDI YA WANANCHI 800 WA WILAYA YA KISARAWE

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Zaidi ya wananchi 800 wa wilaya ya Kisarawe, Pwani wamejitokeza katika zoezi la utoaji wa huduma ya afya bure iliyoandaliwa na madaktari bingwa wa Jumuiya ya Madaktari Watanzania waliosoma China (DCAT).

Akizungumza wakati wa zoezi la hitimisho la zoezi la utoaji wa huduma ya afya bure iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani Dokta Bingwa wa Magonjwa ya Saratani, Dkt Heri Tungaraza amesema kuwa zoezi lao limekuwa la mafanikio makubwa kwa vile wameweza kupata wananchi wengi zaidi.

"Kikubwa tunamshukuru Mungu kwa kuweza kufanikisha zoezi hili na limekuwa la mafanikio zaidi maana tulitarajia watu 400 ila tumepata watu mara mbili ya namba tuliyoiweka, yani tumepata watu zaidi ya 800 na wote tumeweza kuwahudumia japo sisi hatukuwa wengi," amesema.

Amesema kuwa ushirikiano na umoja walionao ndiyo nguzo pekee iliyoweza kufanikisha zoezi walilopanga kulifanya.

"Kiukweli timu yetu imekuwa na ushirikiano zaidi kuanzia Viongozi wa Wilaya ya Kisarawe wakiwemo wafanyakazi wa Hospitali ya Wilaya, waandishi wa habari na wote tuliokuwa nao kipindi hicho," amesema Dkt Tungaraza.

Ameongeza kuwa magonjwa waliyokuwa wakichunguza ni yale ambayo si ya kuambukiza kama vile Shinikizo la damu, presha na idadi kubwa imeonyesha watu wengi wanaugua shinikizo la damu hasa akina mama.

"Tunashukuru waliojitokeza idadi kubwa ni akina mama kwa asilimia 60, akina baba asilimia 30 na watoto asilimia 10% na magonjwa yaliyoongoza baada ya uchunguzi ni Saratani ya Shingo ya Kizazi na Shinikizo la damu na kidogo Kisukari,' amesema.

Ametoa ushauri kwa jamii kuendelea kuchunguza afya zao mara kwa mara ili kuweza kujiimalisha kuliko kusubiri mpaka waugue ndiyo waweze kukimbilia kutibiwa.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Miradi wa DCAT, Linas Kahisha amesema wameshukuru kwa ushirikiano walioweza kuupata kutoka katika serikali ya wilaya ya Kisarawe na pia ubalozi wa China nchini Tanzania ambao ndiyo waliowawezesha kufanikisha zoezi la utoaji huduma ya Afya Bure na pia amewaomba jamii na wadau wengine kuweza kuwaunga mkono ili kufanikisha waweze kufika maeneo mengi zaidi.

"Tumefurahi jinsi uongozi mzima ulivyoweza kutupa ushirikiano kuwezesha wakazi wa Kisarawe kupatiwa matibabu ya afya bure ila japo idadi iliyojitokeza imekuwa ni kubwa nje ya malengo yao waliyokuwa wamepanga," amesema.

Nae Mganga Mkuu wa Halmashauri ya hospitali ya wilaya ya Kisarawe, Stanford John amewashukuru madaktari wa Jumuiya ya Madaktari Watanzania waliosoma China (DCAT) kwa moyo wao wa kujitoa kuhudumia wananchi wa Kisarawe.
 Dokta Bingwa wa Magonjwa ya Saratani, Dkt Heri Tungaraza ambaye ni madaktari bingwa wa Jumuiya ya Madaktari Watanzania waliosoma China (DCAT) akizungumza na wanahabari wakati wa zoezi la hitimisho la zoezi la utoaji wa huduma ya afya bure iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani ambapo amesema kuwa zoezi lao limekuwa la mafanikio makubwa kwa vile wameweza kupata wananchi wengi zaidi. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
 Wananchi wakiojitokeza kupatiwa huduma ya huduma ya afya bure iliyofanyika iliyopita Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani  Mkurugenzi wa Miradi wa DCAT, Linas Kahisha (mwenye miwani) akigawia wananchi maji wakati wa zoezi la hitimisho la zoezi la utoaji wa huduma ya afya bure iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani.
 Dokta Bingwa wa Magonjwa ya Saratani, Dkt Heri Tungaraza (mwenye miwani) ambaye ni madaktari bingwa wa Jumuiya ya Madaktari Watanzania waliosoma China (DCAT) akisimamia utoaji wa huduma ya afya bure.
 Wananchi wakiwa katika dirisha la kupata dawa wakati wa zoezi la hitimisho la zoezi la utoaji wa huduma ya afya bure iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Kisarawe Musa Gama (wa tatu toka  kulia msitari wa mbele) akiwa na  Timu ya Madaktari na wauguzi wa Wilaya ya Kisarawe na madaktari bingwa wa Jumuiya ya Madaktari Watanzania waliosoma China (DCAT).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad