DC IKUNGI AWAONDOLEA HOFU WANANCHI WA KIJIJI CHA MLANDALA MKOANI SINGIDA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 23 September 2019

DC IKUNGI AWAONDOLEA HOFU WANANCHI WA KIJIJI CHA MLANDALA MKOANI SINGIDA

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Mlandala katika mkutano wa hadhara alipofanya ziara ya kikazi juzi kukagua miradi ya maendeleo na kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli kuongoza wilaya hiyo.

DC Mpogolo akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili kijijini hapo.

DC Mpogolo akisalimiana na Mzee Ramadhan Ginza ambaye ni Chifu wa kijiji hicho.

Mkutano ukiendelea.

Wanawake wakiwa kwenye mkutano huo.

DC Mpogolo akiserebuka sanjari na wasanii wa kijiji hicho.

Diwani wa Viti Maalumu (CCM) kutoka Tarafa ya Sepuka, Theresia Masinjisa akizungumza kwenye mkutano huo.

Diwani wa Viti Maalumu (CCM) wa Kata ya Sepuka, Halima Ng'ura akizungumza kwenye mkutano huo.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Hobela Kwilasa akizungumza.

Diwani wa Kata ya Mwaru, Iddi Makangale.

Mwananchi wa kijiji hicho, Musa Kamata akiuliza swali kuhusu sekta ya elimu.

Asha Hassan akiuliza swali kuhusu afya.

Hamza Ntandu akiuliza swali kuhusu vitambulicho vya Nida.

Mzee Iddi Juma akiuliza swali kuhusu malisho ya ng'ombe.

DC Mpogolo akiwa na Mzee Iddi Juma.

DC Mpogolo akipitia nyaraka za ujenzi wa darasa katika Shule ya Msingi Mdughuyu hapo alikuwa akipiga kazi bila ya kujali giza lililokuwepo.

'Wazee ni dawa" DC Mpogolo akiteta jambo na wazee wa kijiji hicho. Kulia ni Mzee Ramadhani Ginza ambaye ni Chifu na Iddi Juma.
DC Mpogolo akikagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mlandala.

Hapa DC Mpogolo, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kata ya Mwaru baada ya kumaliza riaza yake katika kijiji hicho.

Na Dotto Mwaibale, Singida

MKUU wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo amewataka wananchi wa Kijiji cha Mlandala mkoani Singida kuondoa hofu waliyokuwa nayo kutokana na matukio ya kihalifu yaliyojitokeza katika kijiji hicho.

Mpogolo alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na wananchi hao kwenye mkutano wa hadhara alipokuwa katika ziara ya kikazi Kata ya Mwaru ya kukagua miradi ya maendeleo na kujitambulisha kwao baada ya kuteuliwa na Rais Dkt.John Magufuli kuongoza wilaya hiyo.

"Nimesikia kuhusu vitendo vya kihalifu ambavyo vimekuwa vikitokea katika kijiji hiki yakiwemo mauaji nitawasiliana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ili kuzungumzia suala hilo ikibidi mkuu wa polisi wa wilaya afanye utaratibu wa ulinzi" alisema Mpogolo.

Mpogolo alisema serikali haiwezi kuvumilia kuona watu wachache wakiharibu amani ya wananchi huku wakiishi kwa wasiwasi na kushindwa kufanya shughuli zao za maendeleo.

Mkuu huyo wa wilaya alifikia hatua ya kutoa kauli hiyo baada ya wananchi wa kijiji hicho kumueleza kuhusu wasiwasi wa usalama wao kufuatia matukio hayo ya kihalifu na mauaji.

Wananchi hao wakizungumzia matukio hayo walisema yanafanywa na baadhi ya watu kijijini hapo kwa kushirikiana na wageni.

"Watu wanaofanya matukio haya kwa kushirikiana na wageni wanafahamika tunakuomba mkuu wetu wa wilaya utusaidie katika changamoto hii kwani tumefikia hatua ya kuogopa kwenda

kwenye shuguli zetu za maendeleo na kutembea peke yetu nyakati za usiku kuhofia usalama wetu" alisema mkazi wa kijiji hicho Ramadhani Tumbo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad