DAWASA DAR YATAHADHALISHA WAHUJUMU WA MAJI, YASEMA ATAKAYEBAINIKA FAINI YAKE SHILINGI LAKI TANO HADI 50 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 25 September 2019

DAWASA DAR YATAHADHALISHA WAHUJUMU WA MAJI, YASEMA ATAKAYEBAINIKA FAINI YAKE SHILINGI LAKI TANO HADI 50

MAMLAKA ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) imesema watu wote waliojiunganishia maji kwa njia za panya wajitokeze kwenye mamlaka hiyo kwani wakifikiwa faini yake ni shilingi laki tano hadi shilingi milioni 50.

Hayo ameyasema  Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo amesema operesheni hiyo ni endelevu kwa mikoa yote ya Dawasa kutembelea miundumbinu ya maji.

Amesema kuwa operesheni hiyo itakuwa inakwenda kila mkoa na kuwataka wananchi waliojiunganishia maji wajitokeze katika ofisi za Dawasa kufanya utaratibu wa kuunganishwa katika mfumo.

 Zawayo amesema katika maeneo ya Kawe na Msasani wananchi wamekuwa wakitumia maji kwa njia ya udanganyifu na kusababisha hasara kwa DAWASA na kwa wateja halali waliounganishwa na wanaolipa bili.
 Aidha  amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu hivyo ni vyema wanaohujumu miundombinu hiyo wakaacha mara moja kabla ya hatua kali za kisheria dhidi yao hazijachukuliwa.

Zawayo amesema kuwa mmoja wa watuhumiwa wa kuhujumu miundombinu ya maji amekamatwa na atafikishwa mahakani na sheria itafuatwa ili liwe fundisho kwa wengine na wazitumie ofisi za mamlaka hiyo kwa kupata huduma ya maji na sio kuhujumu huduma hiyo kwa wateja ambao wameshalipia huduma zao.

"Tutashughulika  na  wale wote ambao wanahujumu miundo mbinu ya maji na hatutawafumbia macho maana wanasababisha hasara kubwa kwenye mamlaka hiyo kwa kuhudumia maji ambayo hayalipiwi bili" Amesema Zawayo

Amesema kuwa adhabu kwa wahujumu wa miundombinu hiyo ya maji ipo palepale, yaani faini  kuanzia shilingi milioni tano hadi hamsini, na amewashauri wananchi kuwa waaminifu ili kutokutwa na kadhia hiyo.
 Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo(wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa maofisa wa  DAWASA mara baada ya kupatikana kwa mambomba ya maji yaliyokuwa yameunganishwa kinyemela  wakati ukaguzi wa miundombinu ya wakati wa kukagua miundombinu ya maji katika maeneo ya mtaa wa Muzimuni kata ya Kawe jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa Mambo ya Mita kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mohammed Mwakimila(kulia) akimuonesha sehemu ya maungio ya maji yaliyokuwa yanaunganishwa kinyemela kwa Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo(wa pili kushoto) wakati wa kukagua miundombinu ya maji katika maeneo ya mtaa wa Muzimuni kata ya Kawe jijini Dar es Salaam.
Fundi wa DAWASA akipasua sakafu kwa ajili ya kukagua bomba la maji ya Mamlaka hiyo kwenye moja ya nyumba iliyosemekana kuna wizi wa maji wakati wa zoezi la ukaguzi wa miundombinu ya DAWASA leo jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa Mita ya DAWASA iliyokutwa ndani ya jiko la Mteja kabla ya kuvunjwa na kujua kama kuna wizi wa maji wakati wa kukagua miundombinu ya maji katika maeneo ya mtaa wa Muzimuni kata ya Kawe jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa Mita mara baada ya kuvunja sakafu na kujionea wizi mkubwa wa maji ya DAWASA ndani ya jiko la mteja wa Mamlaka hiyo leo wakati wa kukagua miundombinu ya maji katika maeneo ya mtaa wa Muzimuni kata ya Kawe jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya mabomba ya maji yalivyopita kwenye kuta pamoja na sakafuni  yaliyoleta sintofahamu kwenye nyumba hiyo yakiwa yametinduliwa wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya  Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA).
Mfanyakazi wa DAWASA akikagua mabomba yanayoingiza na kutoa maji kwenyw kisima kilichokutwa kwenye moja ya nyumba kwenye mtaa wa Muzimuni kata ya Kawe wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya DAWASA.
Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ukaguzi wa miundo mbinu ya Mamlaka hiyo katika mtaa wa Muzimuni kata ya Kawe jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad