HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 10, 2019

BENKI YA CRDB YAANDAA KONGAMANO LA UWEZESHAJI WAKANDARASI MIRADI YA MAENDELEO NCHINI

Benki ya CRDB imeandaa kongamano maalum la uwezeshaji kibiashara kwa ajili ya Wakandarasi na wadau mbalimbali wa ujenzi wa miradi ya maendeleo nchini ikiwamo ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge Railway) na mradi wa uzalishaji umeme wa bonde la mto Rufiji (Rufiji Hydropower Project).

Akizungumza wakati wa kongamano hilo ambalo lilihudhuriwa na makampuni zaidi ya 400 ya ukandarasi na watoa huduma mbalimbali, Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts alisema kongamano hilo limelenga katika kuwajengea uwezo wakandarasi nchini ili kuwasaidia kutekeleza miradi yao kwa ufanisi zaidi.

“Benki yetu ya CRDB imeweka mikakati mikubwa katika kuhakikisha tunaisaidia Serikali yetu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo, tulianza kwa kutoa mikopo na dhamana katika miradi mbalimbali ikiwamo mradi wa reli ya kisasa ya SGR na mradi wa umeme wa maji wa Rufiji (RHPP). Sasa hivi tumejipanga kuongeza wigo wetu katika kuwasaidia wakandarasi na watoa huduma katika miradi hii, kwani hawa ndio watekelezaji wenyewe,” alisema Dkt. Witts.

Dokta Witts alisema benki hiyo kupitia kauli mbiu yake ya “Tupo Tayari” imejipanga vilivyo kuwahudumia Wakandarasi hao nchini huku akitaja baadhi ya huduma ambazo benki hiyo inazitoa kwa ajili ya wateja kupitia idara yake ya wateja wakubwa.

“Benki yetu sasa hivi inatoa huduma ya dhamana kwa wakandarasi au wateja ambao wanatafuta kazi ijulikanayo kama ‘Bid Guarantee’ hii inatuwezesha kumjengea mkandarasi uwezo wa kupata kazi, lakini vilevile tunatoa dhamana za utekelezaji wa miradi ‘Performance Guarantee’ na dhamana za malipo ya awali ‘Advance Payment Guarantee’,” alisema Dkt. Witts.

Dkt. Witts alisema Benki hiyo imeboresha taratibu zake za utoaji mikopo akiwataka wakandarasi hao kujitokeza kwa wingi kuomba mikopo, pamoja na kujiunga na huduma za bima ili kujikinga na majanga yanayoweza kutokea. “Benki ya CRDB ni Benki yenu, na sisi tupo hapa kuwahudumia niwahakikishie tu sisi Tupo Tayari kuwahudumia,” alihitimisha Dkt. Witts.

Kwa upande wake Msajili Mkuu wa Wakandarasi nchini (CRB), Rhoben Nkori aliipongeza Benki ya CRDB kuwa mstari wa mbele kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini huku akiwataka wakandarasi wote kuchangamkia fursa hiyo inayotolewa na Benki ya CRDB katika kukuza na kuboresha utendaji wa kazi zao.

Wakandarasi na wadau mbalimbali waliohudhuria kongamano hilo waliipongeza Benki ya CRDB kwa hatua hiyo ya kuwakutanisha wadau wa sekta ya ujenzi nchini huku wakieleza fursa zinazotolewa na Benki ya CRDB zitakwenda kuleta sura mpya katika utekelezaji wa miradi ya miundo mbinu nchini.
Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts akizungumza katika Kongamano la uwezeshaji kibiashara lililoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya Wakandarasi na wadau mbalimbali wanaohusika na utekelezaji wa ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo nchini, lililofanyika leo kwenye ukumbu wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Wateja wa Kati na Wadogo wa Benki ya CRDB, Boma Raballah akizungumza katika Kongamano la uwezeshaji kibiashara lililoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya Wakandarasi na wadau mbalimbali wanaohusika na utekelezaji wa ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo nchini, lililofanyika leo kwenye ukumbu wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Mahusiano wa Benki ya CRDB, Tully Ester Mwambapa akizungumza jambo wakati alipokuwa akiongoza Kongamano la uwezeshaji kibiashara lililoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya Wakandarasi na wadau mbalimbali wanaohusika na utekelezaji wa ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo nchini, lililofanyika leo kwenye ukumbu wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya CRDB, Toyi Ruvumbagu akizungumza wakati alipowasilisha mada yake katika Kongamano la uwezeshaji kibiashara lililoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya Wakandarasi na wadau mbalimbali wanaohusika na utekelezaji wa ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo nchini, lililofanyika leo kwenye ukumbu wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa makandarasi nchini, Consolata Ngimbwa akichangia mada katika Kongamano la uwezeshaji kibiashara lililoandaliwa na benki ya CRDB kwa ajili ya Wakandarasi na wadau mbalimbali wanaohusika na utekelezaji wa ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo nchini, lililofanyika leo kwenye ukumbu wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.






























No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad