AKINA MAMA WA MARIA WATAKIWA KULIOMBEA TAIFA NA RAIS JPM - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 29 September 2019

AKINA MAMA WA MARIA WATAKIWA KULIOMBEA TAIFA NA RAIS JPM

Na Mwandishi wetu. 

Mjane Mama Maria Nyerere amewataka akinamama wa umoja wa Maria kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt Magufuli kutoa elimu ya uzalendo kwa Watanzania. Hayo ameyasema hivi karibuni Mke wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mama Maria Nyerere wakati Umoja wa akina mama wenye jina la Maria walipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam. 

 Amesema kuwa ni vyema umoja huo ni kumwombea Rais, viongozi wa serikali na wananchi kwa ujumla ili kuweza kusonga mbele kwa hali ya uzalendo ili kujenfa nchi ikapata matokeo chanya.

"Niwaombe akina mama nyie mliobeba jina langu kuweza kuongeza umoja na mshikamano wenu ili kuweza mambo ya nchi yaende sawa na Afrika kwa ujumla," amesema. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyoya kiserikali ijulikanayo kwa jina la Voice of Orphans Tanzania - VOT, Maria Msaada amesema lengo lao la kumtembelea Mama Maria ni kupata maoni yao ili waweze kusonga mbele. Amesema kuwa wameshukuru kukutana na mama maria nyerere na wapo tayari kufanyia kazi waliyopewa.
Mke wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mama Maria Nyerere akizungumza na akinamama wa umoja wa Maria waliomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam kumjulia khali. 
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyoya kiserikali ijulikanayo kwa jina la Voice of Orphans Tanzania - VOT, Maria Msaada (kushoto) ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha Jina Maria atoa Risala kwa Mama Maria Nyerere walipoenda kumtembelea siku ya Jumamosi.
Mwanachama wa Maria ampa Maria Nyerere zawadi kutoka Chama Jina Maria
Mwanachama wa Maria atoa kitabu cha siri ya rozari kwa Mama Maria Nyerere.
Umoja wa akina mama wenye jina la Maria wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumtembelea Mama Nyerere nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad