HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 30, 2019

Mfuko wa Mazingira kutatua changamoto za mabadiliko ya tabianchi

Serikali imesema Mfuko wa Dhamana ya Mazingira ulioanzishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais utasaidia katika kutatua changamoto mbalimbali za kimazingira zikiwemo mabadiliko ya tabianchi.

Hayo yamesemwa leo Agost 30, 2019 na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mussa Sima wakati akiwasilisha taarifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira.

Mhe. Sima alisema kuwa ni kweli zipo changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya mazingira na Ofisi hiyo imeona ni jambo zuri kuanzisha Mfuko huo utakaosaidia kuimarisha mapato na hivyo kuweza kuzitatua.     

Akitolea majibu kuhusu maoni ya baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo waliopendekeza kuwa taasisi zingine za Serikali zenye uhusiano wa moja kwa moja na masuala ya mazingira zichangie sehemu ya mapato yake kwenye Mfuko wa Mazingira ili uweze kufanya kazi zake.
"Mheshimiwa Mwenyekiti tumeyapokea maoni ya wajumbe wa Kamati hii tutayafanyia kazi na sisi tutakaa na wataalamu wetu tutayaweka vizuri kuyaleta kwenye Kamati hii ili," alisema Naibu Waziri.

Awali katika taarifa hiyo iliyowasilishwa ilibainisha juhudi za Serikali katika kubabiliana na mabadiliko ya tabianchi kuwa ni pamoja na kutekeleza miradi na programu mbalimbali inayosaidia katika utunzaji wa mazingira.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akitolea ufafanuzi hoja mbalimbali katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad