HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 12, 2019

VETA YAJA NA PIKIPIKI SALAMA KATIKA KUKOMESHA AJALI ZA BARABARANI

Na Leandra Gabriel,  Michuzi TV 
KATIKA kuhakikisha ajali za barabarani hasa zile zinazosababishwa na pikipiki zinapungua Mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA) wamebuni pikipiki salama ambayo itahakikisha usalama wa dereva na abiria unazingatia. 

Akizungumza na Michuzi TV mwalimu wa masuala ya umeme kutoka VETA Kipawa Aneth Mganga amesema kuwa ubunifu huo wa pikipiki salama umewalenga madereva na abiria na hiyo ni katika kuhakikisha usalama wao pamoja na abiria unazingatia. 

Aneth amesema kuwa pikipiki hiyo salama imebuniwa kwa kuhakikisha dereva akitumia pombe, akienda mwendo wa haraka, kutovaa kofia ngumu,   kwenda mwendo mkali pamoja na kubeba abiria zaidi ya mmoja pikipiki hiyo haitaruhusu kabisa,  aidha itagoma kwenda au kumpeleka kwenye mwendo wa wastani kama atakuwa kwenye mwendo wa kasi. 

"Pikipiki hii ina mfumo maalumu dereva akinywa pombe,  asipovaa kofia ngumu na akibeba abiria zaidi ya mmoja haiwezi kuwaka na akienda mwendo wa kasi pikipiki hiyo itampeleka katika mwendo wa kawaida" ameeleza. 

Pia amesema kuwa kutokana na mchango mkubwa wa usafiri huo ambao umetoa ajira kwa vijana na kwa kuangalia changamoto zinazoukabili ikiwemo ajali za barabarani wao Kama wataalamu wakaona ni vyema kuangalia namna ya kutatua changamoto hiyo. 

Na amesema kuwa pikipiki hiyo ina mfumo wa usalama ambao utamsaidia dereva kutoa taarifa katika kituo anachofanyia kazi akiona mashaka juu usalama wake juu ya abiria aliyembeba. 

Pikipiki iyo salama imekuwa kivutio kikubwa katika maonesho ya 43 ya biashara maarufu Kama sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Mkufunzi wa masuala ya umeme kutoka VETA Kipawa Aneth Mganga akionesha pikipiki salama ambayo wameibuni ili kupunguza ajali za barabarani, leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad