Na Ali Issa, Maelezo
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imekuwa mshirika mkubwa wa
kimaendeleo kwa Zanzibar katika sekta mbalimbali zikiwemo za kiuchumi
na kijamii.
Hayo yamesemwa huko Hoteli ya Verde na Mkurugenzi wa Idara ya Habari
Maelezo Zanzibar Dkt. Juma Muhammed Salum katika sherehe za miaka 70
ya kuundwa kwa Jamuhuri ya Watu wa China na miaka 55 ya uhusiano wa
Kidiplomasia kati ya China na Tanzania.
Amesema China ilikua ni nchi ya kwanza kuiunga mkono Zanzibar mara
baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964 na ushirikiano huo umekuwa ukiendelea
hadi hivi sasa.
Aliongeza kusema kuwa China imekuwa mstari wa mbele kuisaidia Zanzibar
na kuiletea maendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu,
kilimo, utamaduni na michezo.
Alikumbusha juu ya ujenzi wa hospitali ya Abdalla Mzee Pemba, ujenzi
wa uwanja wa Michezo wa Amanai na Mao tse Tung na kusaidia kuleta
madaktari na vifaa tiba kwa ajili ya Hospitali kuu ya Mnazimmoja na
ile ya Mkoani.
Aidha alisema wameweza kusaidia ujenzi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar
na miundo mbinu ya Barabara na huduma za mawasiliano kwa kuweka taa
katika barabarani mbali mbali za Zanzibar.
Alisema uhusiano uliopo kati ya China na Tanzanzia ni wa kipekee kwani
Rais wa kwanza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mwalimu Julius
Nyerere alikuwa kiongozi pekee alieweza kukutana na Baba wa Taifa la
China Marehemu Mao mjini Beijing mara nyingi zaidi kuliko kiongozi
mwengine yoyote katika uhai wake.
Aidha Mkurugenzi huyo alilieleza kuwa China imekuwa ikitoa elimu kwa
vijana wa Zanzibar katika fani tofauti na imekuwa msaada mkubwa katika
kuimarisha maendeleo ya kiuchumi Zanzibar.
Nae Balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar Xie Xiaowu alisema kuwa Nchi
yake imekuwa rafiki wa kweli na Tanzania na imekuwa mstari wa mbele
kuongeza misaada yake kwa Taifa hilo na Afrika kwa Ujumla .
Aliongeza kuwa China inaendeleza juhudi za upatikanaji wa huduma za
maji safi na salama mijini na vijijini kwa kuchimba visima vipya
katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar na kujenga matangi mapya ya
kuhifadhia maji Saateni na Kilimani.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
Balozi Mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiaowu akitoa hotuba katika Tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Dk,Juma Mohamed Salum akitoa hotuba katika Tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
Balozi Mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiaowu (kulia)akimkabidhi zawadi ya Kitabu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Dk,Juma Mohamed Salum katika tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
Balozi Mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiaowu (katikati)akiwa na Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Dk,Juma Mohamed Salum kushoto yake katika picha ya pamoja na Waandishi wa Habari mbalimbali katika tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
Balozi Mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiaowu (katikati)akiwa na Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Dk,Juma Mohamed Salum wakichukua chakula katika tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
Waandishi wa Habari wakichukua chakula katika Tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Dk,Juma Mohamed Salum
akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza tafrija
maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha
kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde
Maruhubi mjini Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment