HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 15, 2019

RC HOMERA AMPONGEZA MKUU WA WILAYA YA MLELE KWA KASI YA UJENZI WA HOSPITALI, AWAHAKIKISHIA WANANCHI UJENZI WA BARABARA USERVYA KATAVI KWA KIWANGO CHA LAMI

RC Katavi , Mhe. Homera ameipongeza Halmashauri ya Mpimbwe kwa mwenenendo mzuri wa Ujenzi wa Hospitali ya wilaya kwa kufikia 87%.

Aidha, RC Homera amewapongeza kutokana na kasi kubwa ya ujenzi wakiongozwa na mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ndugu Erasto Siwale ,aidha RC Homera amempongeza DED Erasto kwa kuwa msimamizi mahiri wa miradi na kuwaunganisha watumishi kuwa kitu kimoja katika halmashauri hiyo.

Hospitali hii inajengwa kwa Tsh Bilion 1.5. Mhe. Homera amewapongeza pia wafanyakazi na mafundi wanaoijenga hospitali hiyo na kuwataka waendelee kuwa wazalendo na kutotumia saruji na vifaa vingine kinyume na matakwa ya serikali.

Hata hivyo, RC Homera aliwaeleza wananchi waliokuwa hospitalini hapo kuwa ujenzi wa Hospitali hizo za mkoa mzima wa Katavi ni Jitihada za serikali ya CCM ya awamu ya Tano katika kutekeleza ilani yake ya mwaka 2015-2020  ibara ya 49,50 inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli ikisimamiwa vyema na waziri wa Nchi Ofisi Ya Rais Tamisemi Mhe Suleiman Jafo.

RC Homera amewataka wananchi na mafundi kuhakikisha Hospitali inakamilika kwa wakati ili waendelelee kufurahia matunda yanayotokana na serikali ya awamu ya tano.

 Lakini pia RC Homera amewahakikishia wananchi wa Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele mkoani Katavi ujenzi wa barabara kiwango cha lami KM 1.7-Mpaka 2 kwa Bajeti ya  mwaka 2019/2020 Katika Mji wa Uservya chini ya wakala wa Barabara Tanzania ,Tanroad. 

pia hayo yatafanyika sambamba na uanzishwaji wa Benki mojawapo katika mji huo ambao una uzalishaji mkubwa wa mazao ya biashara na chakula pamoja na Kata ya majimoto mkoani Katavi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad