RAIS MAGUFULI KUZINDUA NYUMBA ZA POLISI GEITA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 13 July 2019

RAIS MAGUFULI KUZINDUA NYUMBA ZA POLISI GEITA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amewaomba wananchi wa mkoa wa Geita pamoja na maeneo jirani na mkoa huo kujitokeza kwa wingi siku ya jumatatu kwenye tukio la uzinduzi wa nyumba za Amakazi ya askari, uzinduzi utakaofanyika katika eneo la magogo mkoani humo.

IGP Sirro amesema kuwa, katika tukio hilo ambalo litaongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, ambapo atazindua zaidi ya nyumba 114 zilizokwisha kamilika huku matarajio ya mradi huo ni kuwa na nyumba takribani 400 kwa nchi nzima. 

Aidha, IGP Sirro amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha askari wanaishi kwenye mazingira mazuri jambo ambalo litachangia weledi na uwajibikaji hususan kulinda maisha ya raia na mali zao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad