HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 22, 2019

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MRADI WA UHIFADHI WA CHANZO MAJI KIZINGA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali amezindua mradi wa uhifadhi wa chanzo cha Maji wa mtambo Mtoni kwa kupanda miti aina ya mitomondo na kuweka jiwe la msingi.

Mbio za Mwenge zimetembelea chanzo cha maji cha Mtoni kilichoanza uzalishaji wa maji mwaka 1950 ukiwa na uwezo wa kuzalisha maji kiasi cha ujazo wa lita 7000 hadi 9000 kwa siku.

Kiongozi wa Mbio hizo Mzee Mkongea Ali ameridhishwa na mkakati uliowekwa wa Kulinda vyanzo vya maji kwa kupanda miti na kuwataka wananchi kushirikiana kwa pamoja kuvitunza na kuvilinda.

Amesema, wananchi wanapotunza vyanzo vya maji vinasadia katika kupata maji safi na salama kwa wingi na lengo la Serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt John Pombe Magufuli inalenga katika kumtua mama ndoo kichwani.

Mzee Mkongea, ameweka jiwe la msingi kwenye mradi wa uhifadhu chanzo cha maji cha Mtoni Mashine ya maji na kushiriki upandaji wa miti pembezoni mwa mto.

Akisoma taarifa fupi ya mradi huo, Mkuu wa Idara ya Mazingira wa Mamlaka ya Maji safi na Maji taka DAWASA Modester Mushi amesema, chanzo cha Mto Kizinga kilianza kupunguza uwezo wa uzalishaji wa maji hadi kufikia wastani wa mita 2700 kwa siku kutokana na kukithiri kwa shughuli za kibinadamu ndani ya hifadhi ya mto.

Amesema, wameendelea na juhudi za upandaji wa miti aina ya mitomondo ili kulinda na kuhifadhi chanzo hicho na kufikia Mwaka 2019 miti 10146 imepandwa, pamoja na jitihada za kukutana na wananchi wanaoishi maeneo ya jirani ya mto wanaofanya shughuli za kilimo katika hifadhi ya mto.

"Mpango huu maalumu wa kuhifadhi chanzo cha maji kwa kupanda miti umeleta mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji maji kutoka mita za ujazo 2,700 kwa siku mwaka 2015 hafi kufikia mita za ujazo 7,200 kwa sasa," amesema Modester.

Kwa sasa chanzo cha Mtoni kinahudumia wakazi 480,978 kikiongezeka kutoka 280,000 na lengo ni kuongeza watumiaji wa maji kufikia 751, 978 na idadi hii itafikiwa baada ya kupeleka maji katika tanki la Mbagala kukamilika.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Wa Uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali akiweka jiwe la Msingi katika mradi wa uhifadhi wa chanzo cha maji cha Mto Kizinga na kuunga mkono mradi wa uhifadhi wa vyanzo vya maji kwa kupanda miti baada ya mwenge wa uhuru kutembelea chanzo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Idara ya Mazingira Modester Mushi akisoma taarifa fupi ya mradi wa uhifadhi wa chanzo cha maji cha Mto Kizinga kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali baada ya kutembelea chanzo hicho.

 Mkuu wa Idara ya Mazingira Modester Mushi akikabidhi taarifa fupi kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Wa Uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali baada ya mwenge wa uhuru kutembelea chanzo cha Mto Kizinga leo Jijini Dar es Salaam.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Wa Uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali akipanda mti pembezoni mwa Mto Kizinga ikiwa ni katika kuunga mkono uhifadhi wa vyanzo vya maji baada ya mwenge wa uhuru kutembelea chanzo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Mazingira Modester Mushi akitoa maelezo ya chanzo cha uzalishaji maji kutoka Mto Kizinga kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Wa Uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali baada ya mwenge wa uhuru kutembelea chanzo hicho leo Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad