KAMPUNI YA SKOL BUILDING AGENCY YAKUTWA IKIIBA MAJI YA DAWASA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 13 July 2019

KAMPUNI YA SKOL BUILDING AGENCY YAKUTWA IKIIBA MAJI YA DAWASA

MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam DAWASA wamemkamata mmiliki wa Kampuni  SKOL Building Agency Peter Massawe akiiba maji akijiunganishia kiholela.

Tukio hilo lililotea Jumatatu ya Julai 08, 2019 baada ya kupata taarifa ya mvujo ndipo Moja ya wafanyakazi wa DAWASA kuwasiliana na uongozi na kisha kuanza kufanya uchunguzi.

Akizungumza na Michuzi Blog, Afisa Biashara DAWASA mkoa wa Kawe Jimmy Chuma amesema kampuni hiyo ilikatiwa huduma ya maji toka mwezi April mwaka huu baada ya kuwa na malimbikizi ya madeni yanayofikia 109,718 kwa muda mrefu.

Chuma amesema, baada ya kufika na kuanza kuchimba na kuangalia maji yanapotokea walikuja kugundua, mmiliki huyo alijiunganishia maji kabla ha kufika kwenye mita ya DAWASA na kuendelea kuhujumu shirika.

Ameeleza, baada ya kuona hilo waliwataka wamiliki wafike ofisini kwa ajili ya kupata utaratibu wa kulipa na kutokana na mabadiliko ya sheria namba 5 ya mwaka 2019 mdaiwa atatakiwa kulipa milion 50 au kufikishwa kwenye Vyombo vya sheria.

"Baada ya kufika ofisini tulipowapa taarifa ya kuwa wanatakiwa kulipa milion 50 walisema hawana hela ya kulipa na ndipo leo tumefika hapa kuondoa kabisa miundo mbinu yetu na tayari tumeshatoa taarifa kwenye vyombo husika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua,"amesema Chuma.

Tukio la uchimbaji wa kuangalia sehemu maji yanapovuja yalishuhudiwa na Mona ya viongozi wa Kampuni hiyo Brenda Massawe na mwenyekiti wa serikali ya mitaa.

DAWASA inaendelea kuwasihi wananchi wasijiunganishie maji kiholela pia watoe taarifa kwa kupiga namba ya huduma kwa wateja wanapoona mtu amejiunganishia maji kwani kufanya hivyo kunanyima mamlaka mapato ya kuwezesha kujenga miradi mipya ya maji.
Afisa Biashara, DAWASA Mkoa wa Kawe, Jimmy Jamal Chuma akionesha  akionesha sehemu ilipokuwa mita ya DAWASA  iliyoondolewa kutokana na kutolipa bili za maji lakini Kampuni  SKOL Building Agency iliendelea kutumia maji kwa njia za kughushi bomba.
Afisa Biashara, DAWASA Mkoa wa Kawe, Jimmy Jamal Chuma akionesha moja ya bomba lililowekwa na DAWASCO lilivyokuwa likiingiza maji kwenye Kampuni  SKOL Building Agency mara baada ya kufungwa na Shirika hilona kampuni hiyo kutumia mchepuko kwa kuunganisha bomba kimaghumashi.
Afisa Biashara, DAWASA Mkoa wa Kawe, Jimmy Jamal Chuma akionesha moja ya bomba la maji lililokuwa linatumika kwenye wizi wa maji wa Shirika hilo walipofanya ukaguzi wa kushtukiza kwenye  Kampuni  SKOL Building Agency  iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam.
Moja ya Tanki lililokuwa linatumiwa na Kampuni  SKOL Building Agency kwa kusafishia maji ya DAWASA  yaliyokuwa yanibiwa na kampuni hiyo.
Mmoja wa mafunzi wa DAWASA  akikata bomba linaloingiza  maji katika ofisi ya Kampuni  SKOL Building Agency iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa DAWASA  wakiwa kazini
Sehemu ya Bomba kubwa la maji ya DAWASA  lililokuwa limekatwa na kuingiza maji kwenye ofisi za Kampuni  SKOL Building Agency  iliyopo Sinza Jijini Dar es Salaam likuwa limeishafungwa na DAWASA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad