Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Vickness Mayao akizungumza na vyombo vya habari kuhusu usajili wa Mashirika ambayo hayakusajili kwa Sheria ya NGOs zoezi linaloendelea kwa Kanda ya Kati katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
Mwanasheria wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. January Kitunsi (kushoto) akitoa huduma kwa wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali waliofika katika Kituo cha Usajili wa Mashirika ambayo hayakusajili kwa Sheria ya NGO's zoezi linaloendelea kwa Kanda ya Kati katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
Mwanasheria wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw.
Denis Bashaka(kushoto)akitoa huduma kwa wadau wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali waliofika katika Kituo cha Usajili wa Mashirika ambayo
hayakusajili kwa Sheria ya NGO's zoezi linaloendelea kwa Kanda ya Kati
katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini yanayofanya kazi za kijamii
ambazo awali usajili wake ulifanyika katika Mamlaka nyingine kama
RITA, Msajili wa Jumuiya za Kijamii wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi na BRELA usajili wake utakuwa umefutwa kama zitashindwa
kujisajili chini ya Sheria ya NGO's kama iliyofanyiwa marekebisho na
Sheria Na. 3 ya mwaka 2019 katika kipindi cha miezi miezi miwili toka
tarehe 01 Julai, 2019.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma Msajili wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Vickness Mayao ameyataka Mashirika
hayo kutekeleza matakwa ya Sheria hiyo kwa mujibu wa Sheria na
kuongeza kuwa zoezi linaloendelea la usajili Jijini Dodoma linalenga
Mashirika hayo.
“Sheria inayataka Mashirika hayo kujisajili katika Sheria ya NGO's kwa
kipindi cha miezi miwili hivyo huu ni wakati wa Mashirika kujitahimini
yako wapi ili yaweze kufanya uamuzi sahihi kabla ya kipindi
kilichotolewa na Sheria hii kupita.” Aliongeza Bi. Mayao.
Bi. Mayao amesema usajili huo kwa awamu hii unafanyika kwa mikoa ya
Kanda ya Kati Tabora, Singida, Kigoma na Dodoma na kutoa wito kwa
Mashirika yaliyopo katika Mikoa hiyo kufanya usajili huo akiongeza
kuwa zoezi hili linafanyika bila malipo kwa Mashirika yanayouhisha
usajili lakini Mashirika yanayojisajili mara ya kwanza yanatoa malipo
kwa ajili ya huduma hiyo.
Bi. Mayao ameyataka Mashirika kusajili pia kwa njia ya mtandao kwani
fomu za kujaza zinapatikana kwenye Website ya Msajili ambapo mtu
anayetaka kusajili atajaza fomu hiyo lakini pia kuwasilisha Katiba
dogo ikiwemo sifa za viongozi wa Shirika pamoja na eneo la utekelezaji
au kusudio la shughuli za kazi za shirika.
Aidha Mwakilishi wa Msajili wa Jumuiya za Kijamii kutoka Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi Bw.Thomas Sanila amesema kuwa Ofisi ya Msajili
wa Jumuiya inashiriki usajili huo kuangalia kama kuna mkanganyiko
wowote utakaojitokeza na kufuatilia kama shuguli zinazofanywa na
Shirika husika zinaendana na Sheria na taratibu za Nchi.
Bi. Khadija Omari kutoka Taasisi ya Tuvuke Wote iliyoko Jijini Dodoma
ameyataka Mashirika kujitokeza kwa wingi akisifu taratibu za usajili
kuwa ni za haraka tofauti na alivyofikiria kwani ametumia takribani
nusu saa kukamilisha zoezi la usajili.
Zoezi hili la usajili limeanza tangu tarehe 10 mwezi huu Jijini Dar es
Salaam ambapo asilimia 80 ya NGO's zilizoko Kanda ya Mashiriki
zimefanya usajili wake na zoezi la usajili linaendelea kwa kipindi cha
miezi miwili kama ilivyo elekezwa katika marekebisho ya Sheria Na. 3
ya mwaka 2019.
No comments:
Post a Comment