Benki ya Standard Chartered imezindua kwa mara ya kwanza huduma mpya katika soko la fedha nchini. Uwapo wa bidhaa hiyo ni juhudi za benki kulihudumia soko la fedha kwa njia ya mtandao linalokuja juu kwa sasa.
Huduma hiyo inayojulikana SC Keyboard Banking inatoa nafasi ya matumizi ya mitandao ya simu katika mitandao ya kijamii kupata huduma mbalimbali za kifedha. Huduma hiyo ni sehemu ya mabadiliko makubwa ya utoaji huduma kwa simu kupitia benki ya kidijiti.
Huduma hii ambayo imezinduliwa nchini Tanzania, ipo nchini Kenya, Uganda na Ghana.
Huduma hii kupitia mitandao ya kijamii ni ya kwanza kwa benki katika bara la Afrika na kwamba zinatarajiwa kupelekwa nchini Botswana, Zambia, Zimbabwe na Nigeria kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Watumiaji wa Huduma hiyo watakuwa na uwezo kusafirisha fedha kwa muda huo huo na kufanya malipo mengine na kuangalia salio kwa kutumia mtandao wa kijamii au jukwaa. Upekee wa huduma hiyo ya kidijiti unatokana na ukweli kuwa mtumiaji anaweza kufanya kuwa chaguo la msingi katika simu yake na hivyo kuwa na kasi katika kupata huduma ya kibenki bila kujiingiza katika applikesheni za benki ya kidijiti (SC Mobile App) kupata huduma.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa Wateja wa Kawaida wa Benki hiyo, Bw. Ajmair Riaz, alisema kwamba kuwepo kwa Huduma hiyo ya SC Keyboard Banking ni hatua muhimu katika safari ya kidijiti ya benki hiyo. Alisema kwamba huduma hiyo imebuniwa kwa kuzingatia maslahi ya wateja ambapo wateja sasa wanaweza kulipa tozo mbalimbali, kuangalia akaunti zao na kusafirisha fedha kupitia mitandao ya kijamii iwe ni kwenye Whatsup, Instagram, Facebook, Messenger au njia ya kawaida ya ujumbe mfupi (SMS).
“Tunataka shughuli hii iwe nyepesi na rafiki na kwamba tupo tayari kuendelea kutumia teknolojia ya kisasa ili kuwezesha shughuli za kibenki kuwa za kisasa zaidi na zinazozingatia mahitaji ya wateja.” alisema. Naye Mkuu wa Teknolojia katika benki hiyo Bw. Christopher Vuhahula, alisema wataendelea kuimarisha ubunifu katika teknolojia ya dijiti katika huduma za fedha.
Balozi wa bidhaa hiyo Vanessa Mdee amesema amefurahishwa mno kujihuisha na huduma hiyo na kuwataka mashabiki wake kutumia huduma hiyo kurahisisha maisha yake. “Kama wapenzi wangu mnavyojua, mimi ni mtumiaji mzuri wa simu lakini SC Keyboard Banking ina niruhusu kuendelea kuchati huku naendelea na shughuli zangu za kifedha, imefanya maisha kuwa rahisi zaidi” alisema Vanessa.
Katika masuala ya dijiti Standard Chartered’ ina aplikesheni inayoitwa “SC Mobile Tanzania App” kwa kupitia Playstore au AppStore.
Mkuu
wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi.
Juanita Mramba (kulia) akitoa utambulisho wa meza kuu kutoka kulia kwake
ni Balozi wa Huduma za Kibenki za Kidigitali wa Benki ya Standard
Chartered, Vanessa Mdee, Mkuu wa Wateja wa Kawaida wa Benki hiyo, Bw.
Ajmair Riaz pamoja na Mkuu wa Teknolojia wa benki hiyo Bw. Christopher
Vuhahula wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya SC Keyboard
Banking uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt-Kilimanjaro jijini Dar es
Salaam.
Mkuu
wa Wateja wa Kawaida wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Ajmair
Riaz (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
kuhusu huduma mpya ya SC Keyboard ya Kibenki wakati wa hafla fupi ya
uzinduzi iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar
es Salaam. Katikati ni Balozi wa Huduma za Kibenki za Kidigitali wa
Benki ya Standard Chartered, Vanessa Mdee pamoja na Mkuu wa Mahusiano na
Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba
(kulia).
Mkuu
wa Teknolojia wa wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Christopher
Vuhahula akielezea kuhusu huduma mpya ya SC Keyboard ya kibenki wakati
wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya
Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Wateja wa
Kawaida wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Ajmair Riaz
Balozi
wa Huduma za Kibenki za Kidigitali wa Benki ya Standard Chartered,
Vanessa Mdee (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
kuhusu kupeleka habari njema kwa umma wa watanzania wakati wa hafla
fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya SC Keyboard ya kibenki uliyofanyika
katika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Katikati ni
Mkuu wa Wateja wa Kawaida wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw.
Ajmair Riaz, Mkuu wa Teknolojia wa wa Benki ya Standard Chartered
nchini, Bw. Christopher Vuhahula (kushoto) pamoja na Mkuu wa Mahusiano
na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba
(kulia).
Meneja
Bidhaa wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Ndibalema Rwezaura akielezea
jinsi huduma mpya ya SC Keyboard ya kibenki inavyofanyakazi kwa urahisi
kupitia simu ya kiganjani wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa bidhaa
hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es
Salaam.
Meneja
Bidhaa wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Ndibalema Rwezaura
(kushoto) akijadiliana jambo na wafanyakazi wenzake Meneja Uhusiano wa
benki hiyo, Bi. Mariam Sezinga (katikati) pamoja na Meneja Masoko wa
benki hiyo, Bw. Wilfred Nyakyi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huduma
mpya ya SC Keyboard ya kibenki iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt-The
Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi.
Juanita Mramba (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya SC Keyboard ya
kibenki uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt-Kilimanjaro jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Balozi wa Huduma za Kibenki za Kidigitali wa Benki ya
Standard Chartered, Vanessa Mdee.
Picha
ya pamoja huku fataki zikiwaka kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma mpya
ya SC Keyboard ya Kibenki kwa wateja wa Benki ya Standard Chartered
kutoka kushoto ni Meneja Bidhaa wa Benki ya Standard Chartered nchini,
Bw. Ndibalema Rwezaura, Balozi wa Huduma za Kibenki za Kidigitali wa
Benki ya Standard Chartered, Vanessa Mdee, Mkuu wa Mahusiano na Masoko
wa Benki hiyo, Bi. Juanita Mramba, Mkuu wa Wateja wa Kawaida wa Benki
hiyo, Bw. Ajmair Riaz pamoja na Mkuu wa Teknolojia wa benki hiyo Bw.
Christopher Vuhahula katika hafla fupi iliofanyika kwenye Hoteli ya
Hyatt-Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Picha
ya pamoja kutoka kushoto ni Mkuu wa Teknolojia wa wa Benki ya Standard
Chartered nchini, Bw. Christopher Vuhahula, Mkuu wa Wateja wa Kawaida wa
Benki hiyo, Bw. Ajmair Riaz, Balozi wa Huduma za Kibenki za Kidigitali
wa Benki ya Standard Chartered, Vanessa Mdee pamoja na Mkuu wa Mahusiano
na Masoko wa Benki hiyo, Bi. Juanita Mramba mara baada ya hafla fupi ya
uzinduzi wa huduma mpya ya SC Keyboard ya kibenki iliyofanyika katika
Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wafanyakazi wa benki ya Standard Chartered nchini wakiwa katika
picha ya pamoja na Balozi wa Huduma za Kibenki za Kidigitali wa Benki ya
Standard Chartered, Vanessa Mdee wakiwa na Antu Mandoza wa Radio 7 mara
baada ya hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya SC Keyboard ya
kibenki iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar
es Salaam.
Balozi
wa Huduma za Kibenki za Kidigitali wa Benki ya Standard Chartered,
Vanessa Mdee katika picha ya pamoja na Antu Mandoza wa Radio 7 mara
baada ya hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya SC Keyboard ya kibenki
iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment