HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 6, 2019

Balozi Amina: Bidhaa za viungo hazina ubora katika kupeleka Masoko mbalimbali

 Waziri wa Viwanda na Biashara Zanzibar Balozi Amina Salum akizungumza wakati Siku ya Mwani na Viungo katika Maonesho ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Edwin Rutageruka akizungumza katika siku ya mwani na viungo katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

 Wadau wa mwani na viungo wakiwa siku ya mwani na viungo.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
SERIKALI  imesema bado  bidhaa za viungo na zile zitokanazo na zao la mwani  zinazozalishwa  nchini  hazina ubora stahiki jambo linalosababisha  wazalishaji kushindwa kuzipeleka  katika masoko  mbalimbali  ndani  na nje ya nchi. 

Aidha imesema mdalasini wa Tanzania unahitajika sana duniani,  kutokana na kutokuwa na kiwango cha kemikali na kuwataka wananchi kuchangamkia  fursa  hiyo. 

Kadhalika zao  la Iliki linahitajika kwa wingi  Pakstani ambapo  soko  lake  kubwa Kimataifa. 

Waziri  wa  Viwanda  wa Serikali  ya Mapinduzi Zanzibari, Balozi Amina  Salum  Ali alisema  hayo  jana katika siku  maalum ya bidhaa  za viungo na mwani katika  maonesho  ya 43 ya biashara ya Kimataifa yanayoendelea  katika viwanja  vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa. 

Akizungumza, Waziri Amina  alisema kilimo cha mazao  ya viungo  kina  tija  na kimekuwa  kuwalipa sana na kuhimiza  wazalishaji  kutumia fursa  hiyo  kuzalisha bidhaa  zenye  ubora. 

Alihimiza  wazalishaji kutumia teknolojia ya kisasa na kutaka  vyombo  vya taifa  kuangalia teknolojia rahisi  ya kutumia  yenye  kuwasaidia wananchi. 

Kadhalika alihimiza kuwepo  kwa ubunifu katika  kutengeneza bidhaa zinazotakiwa na hata kuwa  na vifungashio  imara  na bora ili kumudu  soko la ndani na nje  ya nchi. 

Aidha alisema gharama kubwa  za uzalishaji  zinasababisha  bidhaa  kushindwa  kwenda sokoni na kuishauri  Mamlaka  ya Maendeleo  Ya Biashara  nchini  (Tantrade)  kuwezesha wazalishaji  hao  kufikia viwango  vya juu  katika uzalishaji na pia kuondoa changamoto  mbalimbali  wanazokabiliana nazo. 

Awali  akizungumza, Mkurugenzi wa Tantrade Edwin Rutageruka alisema zipo  fursa  mbalimbali  za uzalishaji wa bidhaa  za  viungo na kuwataka  wazalishaji kushirikiana na Mamlaka  hiyo  ili  kuweza kufika  mbali. 
Alisema  wapo  baadhi ya wafanyabiashara  ambao  sio  wakweli  wakiahidi  kusambaza  bidhaa  katika masoko  ya kimataifa lakini  wakiwa  hawawezi  kufanya  hivyo. 

Kuhusu  ushuhuda wa mafanikio  ya bidhaa  za viungo,  Mengi  Sume  aliwataka watanzania  kwa ujumla  kuzalisha  mdalasini  kwa wingi kwa kuwa unahitajika sana na  kemikali kama ilivyo  kwa  mingine. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad