HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 19 June 2019

Mwanza kucheza na Iringa fainali soka wasichana UMISSETA

Kwembe, Mtwara
Timu za Mwanza na Iringa zimefanikiwa kuingia hatua ya fainali baada ya kuwalaza wapinzani wao katika mechi zilizochezwa leo asubuhi katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara.

Katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza bingwa mtetezi Dar es salaam alifungwa na timu ya mkoa wa Iringa kwa magoli 2 kwa 0 na kufuatiwa na pambano la soka kati ya Mwanza dhidi ya Ruvuma ambapo Mwanza iliichakaza Ruvuma kwa magoli 4 kwa 0.

Kwa upande wa soka wavulana mechi  za nusu fainali zilitarajiwa kuchezwa leo jioni ambapo Lindi itacheza na Ruvuma huku Mwanza ikichuana na Songwe.

Katika mchezo wa netiboli timu za Dar es salaam na Tanga zimefanikiwa kuingia hatua ya fainali ambapo mechi za kutafuta mshindi wa tatu na fainali zitachezwa kesho asubuhi katika  viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara.

Timu ya netiboli ya mkoa wa Dar es salaam waliingia hatua hiyo baada ya kuwatoa mabingwa watetezi, timu ya mkoa wa Morogoro kwa  magoli 52-35, huku Tanga ikiifunga Mwanza kwa magoli 45-44.

Wakati huo huo timu za mpira wa kikapu za mkoa wa Mwanza wasichana na Pwani wavulana zimekuwa za kwanza kuingia hatua ya fainali baada ya kuwalaza wapinzani wao.

Katika mechi zilizochezwa leo asubuhi, Mwanza waliifunga Kilimanjaro kwa vikapu 38-28 na kwa upande wa mpira wa kikapu wavulana Pwani waliifunga unguja kwa vikapu 66-32.

Mechi nyingine za kutafuta washindi watakaoingia fainali wanatarajiwa kujulikana jioni ambapo mechi nyingine zitachezwa.
 Winga wa kulia wa timu ya soka ya Mwanza (jezi namba 7) Sharifa Hamidu akijaribu kumtoka beki wa timu ya soka ya mkoa wa Ruvuma Salma Anusa kwenye mpambano wa hatua ya nusu fainali ambapo Mwanza walifanikiwa kuingia fainali baada ya kuibugiza Ruvuma kwa goli 4-1.
 Mshambuliaji hatari wa Mwanza Aaliya Fikiri (jezi namba 8)  akijaribu kuwatoka mabeki wa Ruvuma katika mojawapo ya misuko suko iliyokuwa ikiliandama lango la timu yao 
Lango la timu ya soka wasichana la mkoa wa Ruvuma lilikuwa kwenye misukosuko kwa muda mwingi wa mchezo wa kipindi cha pili ambapo pichani ni Mshambuliaji hatari wa Mwanza Aaliya Fikiri akijiandaa kupiga shuti kuelekea goli hiyo.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad