HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 10, 2019

Mashindano ya John Stephen Akhwari International Marathon kufanyika kila mwaka

Na Shamimu Nyaki -WHUSM
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe ameiyagiza Idara ya Michezo ya Wizara hiyo kushirikiana na Waandaji wa Mashindano ya John Stephen Akhwari International Marathon kufanya mashindano hayo kila mwaka ili kumuenzi Mwanariadha huyo aliyeletea Taifa heshima kubwa. 

Mhe.Mwakyembe ametoa agizo hilo jana Jijini Arusha wakati alipofungua mashindano ya John  Stephen Akhwari International Marathon yaliyofanyika kwa lengo la kutambua na kuenzi mchango wa Mwanariadha huyo ambaye aliitangaza nchi kupitia mchezo huo mwaka 1968 huko nchini Mexico wakati aliposhiriki mbio za Km 42 ambapo licha ya  kuumia goti wakati wa mbio alikataa kusitisha mbio hizo na kuendelea kukimbia hadi alipomaliza kitendo kilichoonekana kuwa ni cha kizalendo kwa nchi yake.

“Serikali inatambua mchango mkubwa uliofanywa na Mwanariadha huyu John Stephen  Akhwari katika mchezo wa riadha ndio maana nimeiagiza Idara ya Michezo kuhakikisha kuwa Mashindano haya yanafanyika kila mwaka ili kuenzi uzalendo wa Mzee Akhwari”.Alisema Dkt.Mwakyembe.
Aidha Mhe.Mwakyembe amewataka wachezaji wote nchini kucheza na kushiriki mashindano mbalimbali kwa lengo la kufaidika katika maisha yao kwakua michezo  katika ulimwengu wa sasa ni ajira hivyo lazima waongeze juhusi zaidi ili waweze kujitangaza ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Riadha nchini Mhe.Antony Mtaka amesema kuwa Mkoa wa Simiyu ambao ndiye anaoungoza kama Mkuu wa Mkoa tayari umeanza kujenga shule maalum ya michezo ili kufundisha vijana wengi zaidi ambao watakuwa na uwezo pamoja na vipaji vizuri katika michezo.
Vile vile Mhe.Mtaka amesema kuwa mchezo wa Riadha umeendelea kufanya vizuri hapa nchini hivyo kutokana na vijana wengi  kujitokeza kucheza mchezo huo na kuahidi kuwa  Shirikisho la Riadha nchini lipo tayari kufundisha wanariadha ambao wapo tayari kujifunza.

Naye Mzee John Stephen Akhwari amewashukuru waandaaji wa Mashindano hayo ambapo amesema kuwa yatasaidia kuongeza ushindani katika mchezo huo,Hata hivyo Mzee Akhwari ameendelea kusisitiza kuwa kila mchezaji anaposhiriki mashindano yoyote nje ya nchi ni lazima atambue kuwa anaiwakilisha nchi yake hivyo ni lazima apambane kwa nguvu zake zote.
Mzee John Stephen Akwari aliingia katika kumbukumbu za Mwanariadha bora na mwenye uzalendo baada ya kushiriki Mbio za Km 42 nchini Mexico ambapo akiwa katikati ya mbio aliumia goti na aliposhauriwa apumzike alikataa na kusema “Nchi yangu haikunituma maili 5,000 kuanza mbio,ilinituma maili 5,000 kumaliza mbio”.

Mashindano hayo  yameshirikisha mbio za Km 21, wanaume na wanawake,Mbio za Km 05 wanaume na wanawake pamoja na Km 2 na nusu kwa watoto ambapo washindi walipatiwa zawadi mbalimbali.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na wanariadha pamoja na wananchi waliojitokeza katika Mashindano ya John Stephen Akhwari International Marathon yaliyofanyika Juni 09 Jijini Arusha yaliyokuwa na lengo la kumuenzi Mwanariadha John Stephen Akhwari ambaye ameletea heshima Taifa mwaka 1968 aliposhiriki mbio za Km 42 nchini Mexico.Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Riadha nchini  ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Antony Mtaka na Kulia ni Mwanariadha huyo Mzee John Stephen Akhwari.
 Rais wa Shirikisho la Riadha nchini  ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Antony Mtaka akizungumza na wanariadha pamoja na wananchi waliojitokeza katika Mashindano ya John Stephen Akhwari International Marathon yaliyofanyika Juni 09 Jijini Arusha yaliyokuwa na lengo la kumuenzi Mwanariadha John Stephen Akhwari ambaye ameletea heshima Taifa mwaka 1968 aliposhiriki mbio za Km 42 nchini Mexico.Kulia kwake ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe.

 Mzee John Stephen Akhwari wa (pili kulia) akionyesha Tuzo ya heshima aliyopewa na waandaaji wa Mashindano ya John Stephen Akhwari International Marathon  yaliyofanyika Juni 09 Jijini Arusha   mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe(mwenye koti jeusi). Wanaoshuhudia ni viongozi wa Shirikisho la Riadha nchini.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akipokea cheti cha utambuzi wa mchango wake katika mchezo wa riadha  kutoka kwa  Rais wa Shirikisho la Riadha nchini  ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Antony Mtaka(kushoto) mara baada ya kumalizika kwa Mashindano ya John Stephen Akhwari International Marathon  yaliyofanyika Juni 09 Jijini Arusha yaliyokuwa na lengo la kumuenzi Mwanariadha huyo ambaye ameletea heshima Taifa mwaka 1968 aliposhiriki mbio za Km 42 nchini Mexico. Kushoto ni Mzee John Stephen Akhwari.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akimvalisha Medali  Mzee John Stephen Akhwari kutokana na mchango wake mkubwa katika mchezo wa riadha hapa nchini mara baada ya kumalizika kwa Mashindano ya John Stephen Akhwari International Marathon yaliyofanyika Juni 09 Jijini Arusha yaliyokuwa na lengo la kumuenzi Mwanariadha huyo ambaye ameletea heshima Taifa mwaka 1968 aliposhiriki mbio za Km 42 nchini Mexico. Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Riadha nchini  ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Antony Mtaka.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akimvalisha Medali  mshindi wa Kwanza wa mbio za Km 21 kwa wanaume  Bw.Emmanuel Giniki katika Mashindano ya John Stephen Akhwari International Marathon yaliyofanyika Juni 09 Jijini Arusha yaliyokuwa na lengo la kumuenzi Mwanariadha huyo ambaye ameletea heshima Taifa mwaka 1968 aliposhiriki mbio za Km 42 nchini Mexico.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akimvalisha Medali  mshindi wa Kwanza wa mbio za Km 21 kwa wanawake Bi.Failuna Abdu  katika Mashindano ya John Stephen Akhwari International Marathon yaliyofanyika Juni 09 Jijini Arusha yaliyokuwa na lengo la kumuenzi Mwanariadha huyo ambaye ameletea heshima Taifa mwaka 1968 aliposhiriki mbio za Km 42 nchini Mexico.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad