Liverpool ndio Mabingwa wa Kombe la Ligi
ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya sita baada ya kuilaza Tottenham katika mechi
ilioshirikisha timu mbili za Uingereza jijini Madrid.
Mohamed Salah alifunga goli la penalti
baada ya dakika mbili kufuatia Moussa
Sissoko aliyeshikishwa mpira na Sadio Mane katika eneo hatari.
Zaidi ya mashabiki 1600 wa Kitanzania, waliweza
kufurahia fursa ya kipekee ya kutazama fainali hizo katika mazingira safi ambapo
miamba wa soka Liverpool kutoka nchini Uingereza walikutana na wapizani wao kwa
ligi ya EPL Totenham Hotspurs. Katika mtanange huo, Liverpool walitawazwa mabingwa
baada ya kuwalaza Totenhan Hotspurs kwa mabao 2-0 .
Ikiwa mmoja wa wadhamini wakuu wa ligi hiyo maarufu na inayotizamwa na
mamilioni ya watu kote duniani, Heineken iliweza kuwaleta pamoja Watanzania chini
ya bia yao pendwa ya Heineken na kupata fursa ya kutazama fainali hizo.
Meneja wa Heineken Tanzania Lungisa Adams alisema, “Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya ni moja kati ya
ligi zinazohusisha wachezaji wakubwa. Timu zote bora barani Ulaya zinashiriki
ligi hii. Kwa upande mwingine, bia ya Heineken ni bia inayojulikana na kutumiwa
na watu wengi kote duniani na kwa hiyo
kuna uhusiano kati ya Heineken na ligi ya mabingwa. Mwaka huu, wateja wetu siyo
tu hawatafurahia kutazama ligi bali pia kushiriki fursa zinazokuja na ligi,”
Lungisa
aliongeza kuwa, wateja wa Heineken waliweza kushiriki pamoja na kubadilishana
taarifa za matukio wakati wakitazama fainali kupitia kibwagizo #ShareUnmissableMoments
“Tunafurahi
kuwa bia ya Heineken ni bia ya Watanzania na siku zote wamekuwa sehemu ya kile
tunachokifanya na hata wanahamu kunywa zaidi bia zetu,” aliongeza.
Wakati wa fainali hizo,
Heineken ilimleta msaniii wa bongo fleva Ray Vanny Kuwafurahisha wateja wake na
pia iliwazawadia bidhaa mbali mbali zinazotokana na ligi hiyo.
Heineken imekuwa mdau wa UEFA tangu mwaka1994
Mwaka
2005, Heineken iliichukua Heineken iliyokuwa inamilikiwa na Amstel
Heineken
italeta udhamini kwa nchi zaidi ya 220 kupitia kampeni za kimasoko na
mawasiliano kwa umma.
Ligi
ya Mabingwa inatazamwa na zaidi ya watu bilioni 4.2 kote duniani.
Tangu
mwaka 2007, kombe la UEFA linalotembezwa na Heineken, limefika zaidi ya nchi 35
ikiwamo Afrika, Asia Amerika ya Kaskazini na Kusini
Kufuatia
kusainiwa kwa mkataba mpya, Heineken itaendea kuidhamini UEFA hadi kufikia
msimu wa mwaka2020/2021.
Mashabiki wa Liverpool wakishangilia kwa msisimko baada ya timu yao kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya sita, wapenzi wa kandanda zaidi ya 1,600 walijikusanya katika ukumbi wa Next Door Arena, jijini Dar es Salaam.
Mashabiki wa Liverpool wa wameshika mfano wa kombe baada ya timu yao kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya sita, wapenzi wa kandanda zaidi ya 1,600 walijikusanya katika ukumbi wa Next Door Arena, jijini Dar es Salaam.
Mashabiki wa Liverpool wakishangilia kwa msisimko baada ya timu yao kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya sita, wapenzi wa kandanda zaidi ya 1,600 walijikusanya katika ukumbi wa Next Door Arena, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment