KMC YAACHANA NA KOCHA ETTIENE NDAYIRAGIJE - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 7 June 2019

KMC YAACHANA NA KOCHA ETTIENE NDAYIRAGIJE

Klabu ya KMC imetangaza rasmi kuachana na kocha wake raia wa Burundi, Ettiene Ndayiragije baada ya kumaliza mkataba klabuni hapo.

Taarifa iliyotolewa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya timu hiyo Benjamini Sitta imeeleza kuwa mkataba wa mwalimu huyo ulimalizika mara baada ya kuhitimishwa kwa msimu wa 2018/19 lakini kocha mwenyewe hakuwa tayari kuongeza mkataba. .

“Baada ya majadiliano ya pande zote mbili, Mwalimu Ndayiragije aliomba kutoongeza mkataba ili aweze kupata changamoto mpya sehemu nyingine. Bodi na uongozi wa KMC umeridhia ombi na matakwa ya mwalimu,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

KMC imetoa shukrani zake kwa kocha huyo kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwa timu msimu huu akiiwezesha kumaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

“Tunamtakia kila lenye kheri katika maisha yake mapya ya huko aendako na uongozi unaendelea na mchakato wa kumpata mwalimu mpya,” imemalizia taarifa hiyo.

Kocha huyo anahusishwa kujiunga na Azam FC, huku tetesi zikieleza kuwa KMC wapo kwenye mazungumzo na kocha wa Lipuli FC Selemani Matola kuchukua mikoba hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad