HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 2, 2019

WAFANYAKAZI WA STAMICO WASHIRIKI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI 2019

* Wakiri Uzalendo na Uwajibikaji ni suluhu katika kukuza Maslahi Bora Sehemu ya Kazi


Na Chalila Kibuda, MICHUZI TV
Wafanyakazi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wameungana na Wafanyakazi wengine nchini kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani mwaka 2019 Kimkoa na Kitaifa ambapo wamekiri uzalendo na uwajibikaji ni suluhu muhimu katika kukuza masilahi bora sehemu ya kazi.

Wafanyakazi hao wa STAMICO wamebainisha hayo katika mahojiano maalum yayoliyofanywa na Michuzi Tv mara baada ya kumalizika kwa Sherehe za maadhimisho Siku ya Wafanyakazi mkoani Dar es Salaam ambapo Kitaifa yaliadhimishwa mkoani Mbeya.

Wamesema Wafanyakazi ni lazima wajifunge mkanda na kuchapa kazi kizalendo, kuimarisha ubunifu na kukuza uwajibikaji, hatua ambayo itasaidia kuinua mapato ya Taasisi zao na maslahi ya watumishi kwa ujumla.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi  ni Tanzania ya Uchumi wa Kati inawezekana, wakati wa Mishahara na Maslahi Bora kwa Wafanyakazi ni SASA.

“Ni wakati muafaka kwa Wafanyakazi kuacha kulalamika na kulaumu Viongozi katika maeneo yetu ya kazi, bali tuchape kazi kikamilifu kwa kushirikiana na Menejimenti ili kutafuta suluhisho la pamoja la kutatua changamoto zetu ili  tutekeleze majukumu yetu kwa ufanisi mkubwa hatimaye tuweze kupata maslahi bora katika kazi.” Alifafanua Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Migodi, Nishati, Ujenzi na kazi nyinginezo (TAMICO) tawi la STAMICO Makao Makuu, Dar es Salaam Bwana Denis Silas.

Akizungumza kutoka mkoani  Mbeya, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa STAMICO Bwana Deusdedith Magala amewapongeza Wafanyakazi kwa ushiriki wao katika Sherehe za Mei Mosi 2019 na amewataka wachape kazi kwa juhudi na maarifa bila manung’uniko; kwani Serikali imetoa dhamana kwa STAMICO kusimamia rasilimali adimu na muhimu ya Madini nchini.

“Kama Mkurugenzi wa Rasilimali na Utawala nasema moshi mweupe kwa STAMICO umeanza kuoneka hivyo kila mmoja wetu achape kazi na kuboresha nidhamu ya kazi ili kukuza ufanisi kwa manufaa mapana ya Shirika na Taifa kwa ujumla. Wakati wa kuonesha matokeo ni sasa hatunabudi kuunga mkono juhudi za Serikali ya Aawamu ya Tano ya kuhakikisha kuwa yananufaisha Taifa.” Alibainisha Bwana Magala. 
 Aidha, Magala ameitaka Menejimenti ya STAMICO kuongeza kasi ya ubunifu na kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati katika Vitengo, Idara na Kurugenzi zao ili kuliwezesha Shirika kutekeleza kwa wakati majukumu yake, ikiwemo miradi yake ya ubia, inayoendeshwa na Kampuni Tanzu na ile inayotekelezwa kwa ushirikiano na Wazabuni.

Alisisitiza kuwa STAMICO kama mwekezaji katika sekta ya madini kwa niaba ya Serikali ina wajibu mkubwa wa kuchangia katika Pato la Taifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad