Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha
SERIKALI ya awamu ya tano imehaidi kushughulikia changamoto za
wafanyakazi kote nchini na kuwataka wawe na subira wakati Serikali ikiendelea
kuzifanyia kazi changamoto hizo na kuwahimiza wafanyakazi kutekeleza wajibu wao.
Akijibu changamoto za wafanyakazi kupitia risala iliyosomwa katika siku ya kilele cha siku ya wafanyakazi duniani iliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Mkuu wa wilaya ya Monduli Iddi
Kimata akimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo amewataka viongozi wa vyama vya wafanyakazi
kupeleka matatizo ya wafanyakazi katika ofisi husika za Serikali ili changamoto hizo ziweze kutatuliwa mara moja.
Aidha ameweka wazi kuwa serikali haitamfumbia macho mwajiri binafsi ambaye atabainika anamnyanyasa mfanyakazi,na iwapo itabainika amemnyanyasa mfanyakazi kwa namna yoyote hatua kali itachukuliwa dhidi take.
"Kuna waajiri ambao wananyanyasa wafanyakazi nimesikia wanawatolea
maneno machafu ,wanawapiga ,na wengine hata kuwanyima haki zao sasa
nasema viongozi wa wafanyakazi naomba hatua kali zichukuliwe na sio hivyo
tu iwapo mwajiri yeyote ambaye atabainika anawanyayasa wafanyakazi
leteni taarifa ili tuwachukulie hatua Kali" alisema kamanta.
Aidha amesema kuwa wiki mbili zijazo kiwanda cha
matairi general trye kitazinduliwa na serikali itaanza mchakato huo na maagizo ya
kuvifuatilia viwanda vingine vilivyofungiwa unaendelea hivyo sherehe za
mei mosi sio siku za kuleta changamoto bali ziwe ni furaha.
"Tukae pamoja kabla ya sherehe tuzungumze mapema na tusingoje hadi
wakati sherehe hizi za wafanyakazi ndio tunaleta changamoto haileti afya kwani sherehe ni furaha na milango ipo wazi kutatua kabla ya
sherehe"amesema kimanta
Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika sherehe za mei mosi Mwenyekiti
Wa chama cha walimu mkoa Wa Arusha Lootha Laizer ameiomba serikali
kuwachukulia hatua Kali waajiri wote ambao wanawanyanyasa
wafanyakazi.
Amesema kumekuwepo na baadhi ya waajiri wa sekta binafsi wamekuwa na
tabia ya kuwanyanyasa wafanyakazi kwa kwa kuwapiga, kuwatolea lugha za
matusi na hata kuwanyima haki zao taarifa zao zimetakiwa haraka iwezekanavyo ili hatua kali ziweze kuchukuliwa.
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi mratibu wa wafanyakazi Mkoa wa
Arusha Samweli Maghero kwa niaba ya wafanyakazi wameiomba serikali kupunguza kodi ya mapato kwa
wafanyakazi kwakuwa kodi hiyo ni kubwa na mshahara ni mdogo ukilinganisha na
hali ya uchumi.
Aidha pia wameiomba serikali kupandisha madaraja (vyeo )kwa wafanyakazi waliokaa
kwa kipindi kirefu bila kupandishwa vyeo ,huku wakiomba serikali
iwape ruhusa ya walimu kuhama vituo vyao vya kazi.
Mratibu wa wafanyakazi Mkoa Wa Arusha Samweli Maghero akisoma Risala kwa niaba ya Wafanyakazi katika kilele cha siku ya wafanyakazi duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Baadhi ya wafanyakazi wakifatilia hutuba ya mgeni
Mwenyekiti Wa chama cha waalimu mkoa Wa Arusha, ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi Mkoa wa Arusha Lootha Laize rakiongea katika maadhimisho hayo ambayo ameiomba Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya waajiri wanaonyanyasa wafanyakazi.
Mkuu wa wilaya ya Monduli Iddi Kimata akihutubia wafanyakazi waliojitokeza kusherekea siku hiyo ambapo amewahimiza kufanyakazi kwa bidii na kuwasilisha matatizo yao kwa wakati.
No comments:
Post a Comment