Waziri wa Elimu nchini Prof. Joyce Ndalichako amethibisha kuunda
kamati itakayoshughulikia namna mkandarasi anayeendelea na ujenzi wa
chuo cha Ufundi Stadi (VETA) mkoani Rukwa alivyopata zabuni na kumtaka
mkandarasi huo ajieleze sababu zilizopelekea kuidanganya serikali
katika mkataba wake ulioonyesha uwepo wa vifaa vya kazi katika eneo la
ujenzi huku eneo hilo likiwa tupu na kazi zake kufanyika bila ya
wataalamu na vifaa vilivyoorodheshwa kwenye mkataba.
Ameongeza kuwa Kamati hiyo pia itashughulikia kuona endapo thamani ya
fedha iliyotolewa na serikali inaendana na majengo yaliyojengwa katika
eneo hilo ambalo yalitakiwa kujengwa majengo 22 ambapo hadi sasa ni
majengo 13 tu kikiwepo kibanda cha mlinzi ndio yameanza kuinuka.
Wakati mkandarasi hiyo akitakiwa kukabidhi majengo hayo mwezi Septemba
2019 hadi sasa ujenzi huo umefikia asilimia 25 tofauti na makubaliano
ya mkataba aliotakiwa kufikia asilimia 61 hadi mwezi Mei.
Katika kuhakikisha wahusika wanashughulikiwa Prof Ndalichako
alimuagiza Mkurugenzi Mkuu wa VETA nchini kuwachukulia hatua wale wote
waliohusika na kumuidhinisha mkandarasi (post qualification) aliyepewa
zabuni pamoja na kumtaka kumchukulia hatua Mkurugenzi wa VETA kanda ya
nyanda za juu kusini kwa kuonyesha kumtetea mkandarasi ambaye hana
uwezo wa kazi.
“Wakandarasi wanaofanya kazi na Wizara ya Elimu badilikeni, kwakweli
miradi yangu yote nitaendelea kuipitia na nitaendelea kuchukua hatua
kali kwa wale wakandarasi ambao wanapata kazi kwa kiujanja ujanja,
kwanza nitashughulika na watu wangu wa kitengo cha manunuzi, hebu
angalia vifaa kama hivyo, kuna Afisa wa wizara ambae anapata mshahara
ate serikali na alikwenda akathibitisha akasema vifaa viko vizuri
akaandika na ripoti, naoma Mkurugenzi Mkuu anza na hao waliofanya
“post qualification” kabla y ahata kamati haijaja kufanya kazi wengine
ambao watakumbwa sasa ni baada ya kamati kufanya kazi, lakini
Mkurugenzi wako wa Kanda hakufai kwasababu anaonekana yeye ni dalali
wa Mkandarasi” Alisisitiza.
Amesema hayo baada ya kutembelea ujenzi wa chuo cha ufundi Stadi VETA
katika eneo hilo la Kashai lililopo katika Manispaa ya Sumbawanga na
kuonyesha kutoridhishwa na kuelekeza kuwa kabla ya kuendelea na ujenzi
huo lazima vifaa vinavyotumika katika ujenzi vipimwe kuonyesha kama
vinastahili ama vinginevyo viondolewe katika eneo la ujenzi na
mkandarasi huyo kuleta vifaa vingine kwa gharama yake.
Awali wakati akisoma taarifa ya ujenzi wa chuo hicho Mkurugenzi wa
Kanda wa chuo cha VETA Justine Rutta alisema kuwa changamoto kubwa
iliyokuwapo ni mkandarasi huyo kucheleweshewa malipo yake na hivyo
anaidai serikali shilingi 51,039,153.59 hali iliyosababisha kuchelewa
kuendelea na ujenzi.
“Kwahiyo kwenye hela nayotakiwa kulipwa inaongezeka deni hilo ambalo
ni kwaajili ya kucheleweshewa ulipaji, hali ya malipo kwa mshauri wa
mradi, ameshalipwa tayari shilingi 1,051,144,000 tangu aanze kufanya
kazi hii na nyingine alitakiwa kulipwa mara atakapofikia hatua ya
kuweka sakafu, kwahiyo hatudai fedha yoyote mpaka sasa, changamoto
katika mradi huu ndio kubwa mradi umeweza kuchelewa kwasababu ya
kuchelewa kulipwa kwa mkandarasi,” alisema.
Katika hatua nyingine, Prof. Ndalichako alibaini uwepo wa kampuni
nyingine mbili zinazohusika na ujenzi wa chuo hicho, kampuni ambazo
serikali haikuingia nazo mkataba na baada yakuulizwa mhandisi wa
ujenzi huo (site engineer) aliyefahanmika kwa jina la Jin alisema kuwa
kampuni hizo zilisaini mkataba na Tender International kwaajili ya
kuwapata vijana wa kufanya kazi, kuwasimamia pamoja na kusimamia
malipo ya vijana hao.
Prof. Ndalichako alisikitishwa na kitendo cha mkandarasi huyo kuingia
mikataba na kampuni nyingine ambazo hazikidhi viwango vya utekelezaji
wa miradi ya serikali kwani kati ya kampuni hizo moja inayoitwa Aricom
Building Constractors limited ilikuwa na daraja 7 na nyingine Laicom
Building Construcors ilikuwa na daraja 4. Na aliyagundua hayo baada ya
kutaka kuonyesha mikataba ya wafanyakazi wa ujenzi huo.
Tarehe 31/8/2019 mkandarasi Tender International alikabidhiwa kiwanja
kwaajili ya kuanza ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) katika
Manispaa ya Sumbawanga ambapo mshauri Elekezi wa Mradi huo ni Sky
Architect Consultancy Ltd na mradi huo kutegemewa kukamillika mwezi
Septemba 2019 huku gharama za mradi huo ikiwa shilingi
10,700,488,940.05 na tarehe 22/11/2018 alilipwa shilingi
1,272,138,424.64. na tarehe 11/4/2019 alilipwa shilingi 835,598,299.01
na kufanya jumla ya Shilingi 2,107,736,723.65 ya malipo kwa Mkandarasi
huyo ambayo ni sawa na asilimia 25 ya malipo yote.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akikagua moja ya gari lililoorodheshwa kwenye mkataba wa ujenzi kuwa ni tipa la tani 7 jambo ambalo ni kinyume na uhalisia.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako na wataalamu mbalimbali kutoka Chuo cha VETA taifa pamoja na Mkoa wakiangalia miongoni mwa matipa 11 yaliyoorodheshwa kwenye mkataba wa ujenzi baina ya Tender Internattional na Chuo Cha Ufundi VETA yakiwa hayafanyi kazi.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce
Ndalichako akimtahadharisha mhandisi wa ujenzi Site engineer)
aliyejilikana kwa jina la Jin ambaye mkataba hauonyeshi mtu huyo
kuhusika na ujenzi huo
No comments:
Post a Comment