HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 6 May 2019

TRFA YATOA MSAADA WA CHUPA 500 ZA DAWA ZA KUTIBU SARATANI KWA WATOTO MUHIMBILI

*Wadau waombwa kujitokeza kusaidia watoto haoNa Karama Kenyunko, globu ya Jamii.

MAMLAKA ya  udhibiti wa mbolea nchini imetoa msaada wa chupa 500 za dawa ya kutibu magonjwa ya saratani kwa watoto ili kuweza kuokoa maisha ya watoto wanaosumbuliwa na tatizo la saratani.

Akizungumza wakati wa kutoa msaada huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka hiyo, Dkt. Stephan Ngailo amesema kuwa dawa hizo zimegharimu Shilingi Milioni 11.

Amesema kuwa, "Msaada huu ni kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli katika kuboresha sekta ya afya na kuwahudumia wananchi ili wawe na afya njema," amesema Dkt. Ngailo. 

Amesema kuwa kwa kuwasaidia watoto hao itawasaidia wazazi wao kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za maendeleo na kukuza uchumi wa Taifa.

"Watoto hawa wakipata matibabu basi muda  mwingi wa wazazi wao utatumika katika kujenga taifa kuliko sasa ambako muda wao mwingi unatumika Hospitalini wakiwauguza watoto" ameeleza. 

Aidha amesema kuwa, "Tunaamini sasa kuwa dawa hii ikitolewa na kutibu  watoto hawa basi wazazi wao watasaidia katika shughuli mbali mbali za maendeleo na kukuza uchumi na pia wanaweza kununua mbolea ili kukuza kilimo na kuongeza uzalishaji na tija na  kuchangia kwenye uchumi wa viwanda kwenye nchi yetu," amesema.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya watoto kutoka hospitali ya taifa  Muhimbili Mary Charles  ameishukuru TRFA kwa msaada wa dawa walizowapatia na amewaomba wadau wengine wajitokeze na kujitolea misaada ya namna hiyo  kwani matibabu ya saratani huwa ni ghali sana.

Amesema dawa wanazotumia kutibu saratani ni za aina nyingi kwa mfano hii Dawa ya Actinomycin inaweza kutumika na dawa nyingine mbili au tatu yenyewe peeke yake hawezi kutibu saratani mpaka iwe na mchanganyiko hivyo wadau mbalimbali wameombwa kujitokeza ili kuwasaidia watoto hao.
 Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya udhibiti mbolea nchini Dkt. Stephen Ngailo (kushoto) akimkabidhi dawa hizo Daktari bingwa  wa magonjwa ya watoto kutoka hospitali ya taifa Muhimbili Dkt. Mary Charles leo jijini Dar  es Salaam.
 Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya mbolea nchini Dkt. Stephen Ngailo akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhi dawa hizo ambapo wadau wameombwa kujitokeza ili kuwasaidia watoto hao, leo jijini Dar es Salaam.
Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto kutoka hospitali ya taifa Muhimbili Mary Charles akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea dawa hizo ambapo ametoa wito zaidi kwa wadau kutoa misaada ya namna hiyo, leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad