HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 28, 2019

TCRA yawafikia Wakazi wa Mafinga katika utoaji wa Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole

Wakazi wa Mafinga na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

 Mkuu wa TCRA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mhandisi  wa TCRA Asajile John amesema ni fursa kwa wananchi wa Mafinga kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa  mawasiliano. 

Amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano. 
Asajile amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe  wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole. 
"TCRA iko karibu na wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo"amesema John.

 Mwananchi akihudumiwa uwekaji wa alama za vidole katika usajili laini za simu wakati wa kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Wananchi wakisoma vitabu vya muongozo vya TCRA mamna ya kutumia bidhaa za mawasiliano wakati wa kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

 Wananchi wa Mafinga na Maeneo ya jirani wakiwa katika Mnada uliokwenda sambamba   na Mnada kwa Mnada karibu tukuhudumia wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) pamoja na wadau mbalimbali katika utoaji wa  elimu wa usajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole.
Wadau mbalimbali wa Mnada kwa Mnada karibu tukuhudumie wakitoa huduma katika Mnada wa Mafinga wakitoa huduma za bidhaa za mawasiliano.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad