NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA
MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo amekemea baadhi ya madiwani kuacha kuingiza siasa kwenye shughuli za wataalamu ,katika
utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa hospital za wilaya unaoendelea
kujengwa kwenye halmashauri tatu za mkoa huo .
Aidha amezitaka, halmashauri zinazojengwa hospital hizo ikiwemo Kibaha
Mji,Kibiti na halmashauri ya wilaya ya Kibaha kuhakikisha wanamaliza
ujenzi huo ifikapo juni 25 mwaka huu .
Akizungumza wakati alipotembelea ujenzi unaondelea katika halmashauri
za wilaya ya Kibaha,Ndikilo aliwataka baadhi ya wanasiasa na watendaji
kukwamisha kwa namna yoyote miradi ya kitaifa na kimkoa kwa maslahi ya
matumbo yao .
Alisema ,katika kukabiliana na changamoto ya utoaji wa huduma ya afya
kwa jamii serikali ya awamu ya tano inajenga hospitali za wilaya tatu
za kisasa ,mkoani hapo ambazo zitagharimu kiasi cha sh. bilioni 4.5.
Ndikilo alielekeza, fedha zote zinazoelekezwa katika miradi hiyo
muhimu zitumike kwa wakati na kwa matumizi lengwa bila kuziacha kubaki
viporo.
"Uzoefu tulioupata kwamba kwanini tunachelewa chelewa sana ni baadhi
yetu kutaka fedha hizi ,hii hii bilioni 1.5 kwa kila halmashauri
wanajiwekea nipate asilimia 10, fundi wangu ,mjomba wangu apate tenda
ya ufundi ,ndugu yangu alete matofali na kutusababishia kuchelewa
malengo yetu"alifafanua Ndikilo.
Nae mkuu wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama alieleza changamoto
kubwa iliyosababisha kuchelewa kidogo kwa ujenzi ni hali ya mvua hivyo
wanaomba kuongezwa muda japo siku 20 badala ya juni 25 mwaka huu.

Awali kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha Suzan Chaula
,alielezea wanajenga majengo saba ambapo ujenzi wa majengo yote
umefikia asilimia 55.
Suzan aliiomba serikali iwaongezee fedha kwa ajili ya ujenzi wa
majengo awamu ya pili na ununuzi wa vifaa kwenye majengo hayo
No comments:
Post a Comment