HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 15, 2019

MMONYOKO WA MAADILI CHANZO CHA UKATILI NDANI YA FAMILIA

Kwa kipindi cha Miezi tisa Julai 2018 hadi Machi 2019 Jumla ya Mashauri ya ndoa 16832 yalipokelewa ikilinganishwa na mashauri 13382 ya mwaka 2017/18 hali ambayo ni sawa na ongezeko la 34% ya migogoro ya ndoa hapa Nchini.

Akiongea kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu Mkurugenzi wa Watoto wa Wizara hiyo Mwajuma Magwiza aliitaja changamoto ya maadili ya mmomonyoko wa maadili kuwa chanzo cha migogoro ya ndoa hapa Nchini.

Magwiza aliongeza kuwa Vitendo vya ukatili kwa watoto ndani ya familia vimekithiri huku wahausika wakubwa wa vitendo hivyo wakiwa wanafamilia hili likijionesha katika takwimu za Jeshi la polisi za mwaka 2017 zinaonesha kuwa Jumla ya matukio ya ukatili kwa watoto 13457 yameripotiwa na Jeshi la polisi.

Alivitaja vitendo hivyo kuhusisha ukatili wa kingono wenye matukio 3,583, mimba za utotoni 1,323 akiongeza kuwa taarifa jeshi hilo imeonesha matukio ya mikoa ya kipolisi yenye ukatili mkubwa kuwa ni kinondoni matukio 2,426, Dodoma 1,283, Tanga 164, Tameke 984 na Arusha Matukio 972.

Wakati huo huo Serikali imewataka baadhi ya Wazazi Nchini kuacha tabia ya kutoa kipaumbele cha elimu kwa watoto wa kike kama ilivyo kwa watoto wa kiume jambo ambalo linakwamisha juhudi za Serikali katika kuhakikisha usawa wa kijinsia unatekelezwa katika nyanja zote bila ubaguzi wa kijinsia.

Akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhandisi Happiness Mgalula ambaye pia ni Katibu Tawala Masaidizi Mkoa wa Dodoma aliongeza kuwa ni lazima elimu itolewe kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.

Aidha Mgalula amewataka wazazi na walezi kutoa kipaumbele cha elimu kwa watoto wote bila kujali jinsia ikiwa ni hatua muhimu ya kutekeleza ahadi ya Rais kwa vitendo ya utoaji elimu bure kwa wanafunzi hapa Nchini.

Mgalula aliongeza kuwa Tanzania bado inakabiliwa na tatizo la mila potofu akizitaja mila hizo kuwa ni kuwa ni mimba na ndoa za utotoni, haki ya wanawake kumiliki ardhi, vipigo kwa wanawake akiutaja mkoa wa Dodoma kuwa wa pili kitaifa katika vitendo vya ukatili hapa Nchini.

Aidha Mugarula amewataka wanafamilia kuhakikisha wanakuwa ana Afya bora kwa kuhakikisha wanakuwa na vitambulisho vya Bima ya Afya, Elimu na akina mama wajawazito kuhakikisha wanaenda hospitali ili kupata huduma ya Afya kwa mama na mtoto.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dodoma Happy Hiza amesema Mkoa wa Dodoma umefanikiwa kutoa elimu juu ya Makosa ya Jinai kwa maafisa Ustawi na Maendeleo ya jamii na katika ngazi ya Jamii ili kuwezesha elimu ya malezi na makuzi kwa watoto katika jamii.
 Wanafunzi wa kikundi cha Brass Band kutoka Shule ya Msingi St. Home wakiongoza Maandamano ya Wanafunzi wenzao katika kilele cha Mazimisho ya Siku ya Familia Duniani yaliyofanyika leo katika Mkoa wa Dodoma.
 Mkurugenzi wa Idara ya Watoto wa Wizara ya Afya kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Mwajuma Magwiza akitoa hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara yake wakati kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani yaliyofanyika leo katika Mkoa wa Dodoma.
 Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma Happiness Mgalula akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakati wa kilele cha Mazimisho ya Siku ya Familia Duniani yaliyofanyika leo katika Mkoa wa Dodoma.
 Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma Happiness Mgalula akivalishwa skafu na Skauti wa Mkoa wa Dodoma mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Nyerere Square katika Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani .
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma Happiness Mgalula akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad