HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 6 May 2019

MKURABITA YAHIMIZA KILIMO BIASHA KWA WAKULIMA WA UYUI

NA TIGANYA VINCENT
WAKULIMA wilayani Uyui wamehimizwa kujiunga na kilimo cha kisasa na kibiashara ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kujiongeze kipato kwa ajili ya maendeleo ya familia zao na Taifa kwa ujumla.

Pia wametakiwa kujiunga na Taasisi za fedha ili waweze kupata mikopo itakayowawezesha kulima kilimo cha kibiashara.

Kauli hiyo imetolewa jana na Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu wakati wa kuhitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima 100 na viongozi 10 wa Kata ya Miyenze wilayani Uyui.

Alisema kilimo biashara ndio kitaweza kuwakwamu kiuchumi wananchi na kuondokana na umaskini na kuwataka wakulima ambao wamesharasimisha ardhi zao kuwa na mashamba darasa ya kilimo biashara ili wawe chachu ya mabadiliko kwa wengine.

Meneja huyo alisema kwa wakulima ambao tayari aridhi zao zimerasimishwa ni rahisi kukopesheka kwa kuwa wanazo hati na baadhi yao wameshaunganishwa na Benki mbalimbali.

Temu alisema ni vema wakulima hao wakatumia hati zao kutafuata mikopo ambao itawaondoa katika kilimo duni na kugeuza kuwa kilimo ambacho kitaleta mapinduzi katika maisha yao.

Aliwataka wakulima walijengewewa uwezo kuwa na mashamba darasa ya kilimo biashara ili wakulima ambao hawakupata fursa hiyo waende kujifunza kwao.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya alisema kuwa mpango wa wilaya hiyo ni kuhakikisha kila kaya inalima ekari tatu za mazao ya biashara pamoja na mazao mengine ili kuwawezesha wananchi kujiongezea kipato. Alisema mazao hayo ni pamoja na tumbaku, pamba, korosho na alizeti.
 Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu akisoma maazimo ya mafunzo wakati wa kufunga jana mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima 100 na viongozi 10 wa Kata ya Miyenze wilayani Uyui.
Afisa Tafiti na Ufuatiliaji kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) Francis Mjuni akitoa elimu jana kwa wanakijiji wa Miyenze wilayani Uyui waliopata hati miliki za kimila juu ya umuhimu wa utunzaji wa kumbukumbu katika shughuli mbalimbali. 
 Baadhi ya wakulima wa Kata ya Miyenze wilayani Uyui wakipata maelezo juu ya umuhimu wa kilimo biashara kutoka kwa Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini wa Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu (hayupo katika picha) wakati wa kuhitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima 100 na viongozi 10 wa Kata hiyo.
 Baadhi ya wakulima wa Kata ya Miyenze wilayani Uyui wakinyosha mikono juu kuunga mkono maelezo ya kuwahimiza juu ya kilimo biashara yalikuwa yakitolewa na Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini wa Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu(aliyesimama kati kati yao) wakati wa kuhitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima 100 na viongozi 10 wa Kata hiyo. Picha na Tiganya Vincent RS Tabora   

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad