HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 7 May 2019

MILVIK, TIGO PAMOJA NA RESOLUTION INSURANCE KUWAPATIA WATANZANIA BIMA YA AFYA KWA BEI NAFUU

Wa kwanza kushoto ni Melchizedek Nyau - Meneja Uendeshaji Resolution Insurance, Hussein Sayed - Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Zamaradi Mketema - Balozi wa Milvik Tanzania 

Tigo kwa ushirikiano na Milvik Tanzania na Resolution Insurance tumeungana na mwanahabari mashuhuri na mama wa watoto watatu, Zamaradi Mketema, kuzindua Bima mkononi ya kulazwa na watoto kwa wateja wa Tigo pesa. Huduma hii inawapatia watumiaji wa Tigo Pesa bima nafuu inayowalinda wao na watoto hadi watano kwa sh.750 kwa mwezi kwa kila mtoto.

Wateja wa Tigo pesa wenye umri wa miaka 18 - 64 kwa sasa wanaweza kuongeza watoto wao wenye umri kuanzia Mwaka 1 hadi miaka 17, kwenye Bima Mkononi yao ya kulazwa na mtumiaji atapokea Sh. 40,000 kama fidia kwa kila usiku atakaolazwa hospitali.

Huduma hii nafuu sana kwa Sh. 1,500 tu kwa mwezi kwa mteja mwenyewe na ongezeko la Sh 750 kwa kila mtoto. Malipo moja kwa moja kwenye akaunti ya Tigo pesa ya mtumiaji kila mwezi hivyo hii kumpunguzia mtuamiaji mzigo wa kufikiria kufanya malipo. Malipo ya fidia hutumwa moja kwa moja kwenye akaunti Tigo pesa ya mtumiaji.

Berengere Lavisse, Meneja Mkuu wa Milvik: "Toka tumezindua huduma ya kulazwa mwaka 2016, wateja wetu wamekuwa wakituomba kuboresha huduma zetu na kujumuishawatoto kwa bei nafuu; tumesikiliza mahitaji ya wateja wetu na kwa kushirikiana na wadau wetu pamoja na Mamlaka ya udhibiti wa bima Tanzania (TIRA), tumefanyia kazi kuleta huduma hii ya bima ya kulazwa kwa watoto. shirikiano wetu na Tigo unatuwezesha kuwafikia watu wengi zaidi hususani kwa watumiaji wa Tigo, ushirikiano huu ni muhimu kwetu katika kulinda hatima za familia nyingi zaidi. . Tuna furaha kubwa kuwa na ushirikiano na Zamaradi kama balozi wa huduma zetu.Kama mama mchapakazi anaelewa umuhimu na uhitaji wa kuwalinda uwapendao”.

Zamaradi Mketema, Balozi wa Bima Mkononi alikuwa na haya ya kusema, "Kama mama ninawajali watoto wangu, natamani kina mama na kina baba wote Tanzania wapata uwezo wa kutumia bima rahisi na nafuu zinazolinda familia zao na hiki ndicho Bima Mkononi ya kulazwa na watoto inachokitoa. Kuwa na watoto wadogo watatu inanifanya niwe na majukumu muda wote, kwahiyo kuwa na huduma rahisi kujisajili, rahisi kulipia na pia rahisi kufanya madai, ni fursa muhimu sana kwangu”.

Hussein Sayed, Afisa Mkuu - Huduma za Kifedha Tigo: "Kama sehemu ya jitihada zetu za dhati kabisa katika kuwaelewa wateja na kufanya maboresho yanayoendana na mahitaji yao kijamii, tumeungana na IDEO.org, katika utafiti wa jinsi tunavyoweza kuongeza ushiriki wa jamii katika huduma za kifedha na hususani kwa wanawake na kaya, matokeo ya utafiti huu yanaendana na mfumo ambao umeundwa na timu ya Milvik...Hivyo , ninafurahi kutangaza maboresho ya huduma za Bima Mkononi kwa wateja wetu wapendwa, inayotolewa kwa viwango nafuu na ambayo ni rahisi na ya haraka kujiunga. Tigo imejidhatiti katika mpango mkakati kuongeza ushiriki katika huduma za kifedha, ambapobima ni kiungo muhimu katika kufanikisha hilo. Tunajivunia kusema kuwa tumechukua hatua nyingine mbele zaidi, si tu kulinda maisha ya wateja wetu, bali pia maisha ya wale wawapendao”.

Melchizedek Nyau, Meneja uendeshaji Resolution Insurance: "Kama wadhamini wa bima hii, lengo letu ni kulinda kila chenye thamani kwa wateja wetu kwa kuhakikisha tunatoa huduma zenye tija, , za kuaminika, sahihi, na zenye uwazi. Toka kuanzishewa kwa bima ya kulazwa mwaka 2016 tumekuwa tukitimiza ahadi yetu ya kulipa madai kwa haraka ndani ya siku 3 hadi siku 5”.

Usambaaji wa bima nchini Tanzania ni mdogo ikiwa ni asilimia 1 tu ya Watanzania wenye huduma za bima, na bima ikichangia asilimia 0.9 tu kwenye kipato cha ndani cha taifa. Milvik, Tigo na Resolution Insurance tumejidhatiti katika kuchangia kwenye mfumo wa kuingiza fedha wa taifa (Tanzania National Financial Inclusion Framework (NFIF 2018-2022) ili kutoa huduma za kifedha zinazowajali wateja na kukidhi mahitaji yao ili kuboresha hali ya maisha yao ,pamoja na kuendelea kuwaelimisha watu wenye kipato cha chini jinsi bima inavyofanya kazi, sambamba na sera ya taifa ya elimu juu ya maswala ya bima (NATIONAL INSURANCE EDUCATION STRATEGY (2016 - 2020). Huduma za bima za Bima Mkononi ni rahisi - zinazokidhi mahitaji ya watu wenye kipato cha chini ambayo bima nyingine hazijaweza kukidhi mahitaji hayo, yaani kutoa huduma zenye vigezo na masharti rahisi ambayo ni rahisi kueleweka.

Kujiunga na Bima Mkononi ni rahisi. Wateja wanaweza kujisajili kupitia simu zao za mkononi kwa kutumia USSD kwenda nambari *148*15# au kupitia mawakala wa huduma kutoka Milvik kwa kupiga simu ya bure kwenda nambari 0659071001. Madai halali yanaweza kutumwakupitia whatsapp, barua pepe au kupelekwa kwenye tawi la Tigo kwa kutuma fomu ya taarifa fupi ya kuruhusiwa kutoka hospitalini na cheti cha kuzaliwa, na madai yatalipwa ndani ya siku tatu za kazi baada ya kupokea nyaraka halali.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad