HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 27, 2019

Madereva fuateni sheria za usalama barabarani kupunguza ajali - Samwix

Na Chalila Kibuda, Blog ya Jamii
Ajali za barabarani zinaweza kupungua au kuisha   kutokana na madereva kukubali katika kufuata kanuni pamoja na sheria za usalama barabarani katika uendeshaji wa mabasi ya mikoani na nje ya nchi jirani.

Akizungumza na Madereva wa Mabasi ya Mikoani na nchi jirani Mkuu wa Kituo cha Ukaguzi wa Mabasi na Magari cha Ubungo jijini Dar es Salaam Ibrahim Samwix wakati akitoa mafunzo kwa medereva wa mabasi ya mikoani na nchi jirani  yaliyofanyika katika kituo cha Ofisi za Ukaguzi  majira ya saa 11 alfajiri jijini Dar es Salaam.

Samwix amesema kuwa madereva wakifata kanuni za kidereva  kwa kufuata matakwa yaliyowekwa basi ajali zitapungua au kuisha kabisa.

Samwix amesema kuwa taratibu zilizowekwa kwa mabasi yanayokwenda zaidi ya masaa nane kuwa na madereva wawili lakini kuna watu wanakuwa na madereva wasio na sifa 'Bosheni' ambapo ni kosa la sheria kwa dereva kuwa na dereva asiokuwa na sifa za udereva.

Amesema kuwa madereva waonyeshe ushirikiano  mara baada ya kuona dereva mwenzao hana mtu wa pili kutoa taarifa katika kituo cha  ukaguzi Ubungo ili kuweza kuwachukulia sheria kwa dereva kuruhusu kukaa na dereva wa pili asiyekuwa na sifa bosheni.

Aidha amesema kuwa mafunzo wanayoyatoa kwa madereva ni endelevu ii kufanya kazi hiyo kwa kujitambua pamoja na kuepuka na ajali ambazo zinauwezekano kukwepeka kutokana na ustadi wa udereva.

Amesema kuwa mafunzo hayo wakijua wataweza kuwa mabalozi wa madereva wengine kwa kueleza mbinu mbalimbali za uendeshaji wa mabasi kwa kuangalia masilahi ya abiria.

"Teknolojia  ya mabasi inabadilika hivyo lazima madereva wa mabasi wa wabadilike ikiwa ni pamoja na kupata mafunzo ya namna ya kuendesha magari kwa kisasa na sio mazoea ya udereva wa mwaka 1940"amesema Samwix.
 Mkuu wa  Kituo cha Ukaguzi Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo INSP. Ibrahim Samwix akiwafundisha madereva wa mabasi ya mikoani na nchi jirani mamna ya kuepuka ajali wakati gurudumu limepasuka katika mafunzo ya madereva Katika kituo hicho.
 Mkuu wa Kituo cha Ukaguzi cha Ubungo Ibrahimu Samwix akitoa mafunzo madereva wa mabasi ya mikoani na nje ya nchi kwa ajili ya kujitambua katika kazi yao ya Udereva.
Madereva wakiwa katika mafunzo  katika kituo kikuu cha mabasi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad