Na Ahmed Mahmoud Arusha
Serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani Idara ya uhamiaji imekanusha
taarifa zilizosambaa kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandao
kijamii kuwa idara hiyo inapokea malipo mkononi kutoka kwa wateja
wakati inafamika malipo yote ya serikali hulipwa kwa njia za huduma za
kifedha.
Kamanda wa Idara ya Uhamiaji mkoani Arusha Mratibu msaidizi Samwel
Mahirani ameyasema hayo alipokuwa akiongea na vyombo vya habari
ofisini kwake na kuwataka watanzania kuwaamini viongozi wao na kutoa
taarifa za malalamiko bila woga
Amekemea vikali wale wote wanatumia mtandao kuichafua Idara hiyo
kuacha mara moja na pia kutoa taarifa kwa uongozi pindi wanapoona hawa
kuridhishwa na huduma kwani kuna vitengo mbali mbali na box la maoni
haoni sababu ya kulizungumza mtandaoni.
“Taasisi zote za umma hazipokei fedha mkononi bali fedha zote za umma
zinapokelewa kwa njia ya miamala ya kifedha ikiwemo benki na mitandao
ya simu za mkononi” alisema Kamanda
Alisema kuwa Hapendezwi na wanaotumia mitandao ya kijamii kuichafua
Idara hiyo kwa kusema wanachukuwa rushwa na kupokea fedha mkononi hilo
sio sahihi walitakiwa kufika ofisini kwangu na wakiona hawawezi
kuniona basi kuna taasisi za kupambana na kuzuia rushwa badala ya
kukimbilia huko.
Amesema Idara hiyo mwaka 2018 wamefanya misako na doria Zaidi 234 na
kukamata wahalifu 96 waliofikishwa mahakamani ambapo 128 kutoka
mataifa mbali mbali waliondoshwa nchini
Amebainisha kuwa Jumla ya Pasi kubwa za kusafiria 1384 zimetolewa
tokea Dec hadi mei mwaka huu sanjari na pasi ndogo 14,183 ambapo idara
ya uhamiaji mkoani hapa imezitoa kwa wananchi wanaosafiri nje ya nchi.
Alieleza kuwa wahalifu 314 kati yao 38 walipandishwa mahakamani ambapo
86 waliondoshwa nchini ambapo Idara hiyo imetoa angalizo kwa askari
wake wenye tabia hizo kuacha mara maja kwani.
Akatoa wito kwa wananchi kutoa taarifa pindi wanapoona vitendo viovu
na kuacha kutumia mitandao ya kijamii ili na wao kuweza kuboresha
huduma zao kwani maoni yanasaidia kuliko kutoa malalamiko kwani
hayajengi.
No comments:
Post a Comment