Waumini wa Dini ya Kiislamu Nchini wanaendelea na harakati zao za
kufutari pamoja zinakopelekea kushibana kiimani ya moyo ndani ya
Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, mwezi ambao umeteremshwa Kitabu
Kitakatifu cha Quran kisichoshaka katika kubainisha Haki na Batil.
Futari hizo zinazojumuisha Waumini wa rika tofauti ufanywaji wake
hupaswa kuzingatia utaratibu maalum wa hali ya Kiafya na Mazingira
safi uliowekwa na Uongozi wa Manispaa pamoja na Halmashauri za Wilaya.
Futari hiyo iliyoandaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi iliwahusisha Wazee wanaohifadhiwa kwenye Nyumba za
Serikai Sebleni pamoja na Wazee wa Chama cha Mapinduzi wa Mkoa wa
Kaskazini Unguja na kufanyika katika Ukumbi wa Nyumba za Wazee Sebleni
Mjini Zanzibar.
Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed alisema Balozi Seif bado
anaendeleza tabia njema ya kuwashirikisha Wananchi mbali mbali katika
Futari ya pamoja.
Waziri Aboud alisema kitendo cha kufutarisha ni maamrisho ya Mwenyezi
Muungu aliyoawaagiza Waumini wake wenye uwezo kuwasaidia Waumini
wenzao wenye maisha duni ili kuwaunganisha katika futari hiyo ambayo
ni matendo anayoyafurahia Allah Subuhanahu wataala.
Mjumuiko wa kufutari kwa makundi ni utaratibu aliyojipangia Balozi
Seif wakati anapopata wasaa wa kufanya hivyo katika muelekeo wa
kuwashirikisha Wana Jamii kwenye mjumuiko huo wenye kuleta ushirikiano
miongoni mwa Wananchi mbali mbali Nchini.
Baadhi
ya Wazee wanaoishi katika Nyumba za Serikali Sebleni Mjini Zanzibar
waki katika Futari ya pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud
Mohamed akitoa shukrani kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
mara baada ya futari ya pamoja na Wazee wa Nyumba za Serikali Sebleni.
Balozi
Seif akibadilishana mawazo na baadhi ya Wazee Wanaume wanaoishi nyumba
za Serikali Sebleni mara baada ya kufutari nao pamoja iliyowashirikisha
pia baadhi ya Wazee wa Chama Mkoa Kaskazini Unguja.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na baadhi ya
Wazee Wanawake wanaoishi nyumba za Serikali Sebleni mara baada ya
kufutari nao pamoja iliyowashirikisha pia baadhi ya Wazee wa Chama
Mkoa Kaskazini Unguja.
Picha na – OMPR – ZNZ.
No comments:
Post a Comment