HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 26, 2019

Vijana 200 kuhudhuria mkutano wenye mfumo kama Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Morogoro


ZAIDI ya vijana 200 kutoka nchini na nje ya nchi wanatarajia kuhudhuria mkutano mkubwa utakaoendeshwa kwa mfano wa mfumo wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kisheria na kikanuni.

Mkutano huo utakaofanyika Morogoro unatambuliwa kimataifa kama Tanzania International Model United Nations (TIMUN) unajumuisha vijana kuanzia miaka 15-30.

Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari, mratibu wa tukio hilo Bw. Kelvin Edward alisema: “Nimefurahishwa sana kuona washiriki wengi wa tukio la mwaka huu wanataka kuhakikisha kwamba vijana wa leo na kesho wanawezeshwa . Nashukuru sana mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa kuwezesha jukwaa la vijana kubadilishana mawazo kuhusu utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu kufikia mwaka 2030. Katika mkutano huo vijana watapata nafasi ya kubadilisha mawazo  na kuelezea matumaini yao .”

Mkutano wa mwaka huu utazingatia zaidi kuangalia maendeleo endelevu (SDGs). majadiliano yatalenga zaidi ushiriki wa vijana katika kipengele cha tatu cha SDG kinachogusa Afya na ustawi; Kipengele cha nane kazi zenye staha na ukuaji wa uchumi; kipengele cha 13 mabadiliko ya tabia nchi na kipengele cha 16 cha amani, haki na taasisi zenye uwezo .

Akizungumza kwa niaba ya Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa , Msemaji wa umoja huo kitaifa, Bi. Didi Nafisa  amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia vijana katika utekelezaji wa SDGs.  “Vijana wanafanya idadi kubwa  ya wananchi. Ni muhimu kwa wao kupewa taarifa na pia kuhusishwa na utekelezaji wa malengo ya  maendeleo endelevu hasa kwa sasa ambapo kinachoangaliwa zaidi ni matokeo.”

TIMUN  inaendeshwa na Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA), na hufanyika  kila mwaka kwa vijana kuletwa pamoja kutoka mataifa mbalimbali duniani .

Akizungumza na mwenyekiti wa YUNA Bw. Jolson Msaki amesema matukio  kama ya TIMUN yanaleta vijana karibu na Umoja wa Mataifa na kuongeza uwezo wa vijana kujadili masuala yanayogusa dunia na kupata fursa ya kutoa suluhu ya utekelezaji wa  SDGs .


Tukio la mwaka huu limedhaminiwa na Umoja wa Mataifa Dar es salaam, ofisi ya Waziri Mkuu, UNICEF, UNFPA, UNIC, Ubalozi wa Marekani, Pathfinder, Plan International na International Youth Foundation.
Mratibu wa TIMUN 2019, Kevin Edward (kulia) akitoa maelezo kuhusu namna vijana wanavyonufaika na Mkutano wa vijana unaoendeshwa kwa mfumo wa Mikutano ya Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Habari wa Umoja wa Mataifa, nchini Bi Didi Nafisa.
Ofisa Habari wa Umoja wa Mataifa nchini, Bi Didi Nafisa akielezea namna ambavyo vijana wanavyokutanishwa kujadili namna ya kutekeleza vipengele vya maendeleo endelevu (SDGs) kwa kuwasilisha hoja za kitaifa; na namna Umoja wa Mataifa unavyosaidia makundi ya vijana kufikia usitawi wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa YUNA Tanzania, Bw. Jolson Masaki (kushoto) akitoa ushuhuda namna TIMUN inavyosaidia vijana. TIMUN hufanyika mara moja kwa mwaka na hii ni TIMUN ya 22. Katika mkutano huo vijana hujadiliana kuhusu mambo mbalimbali ya duniani na kutoa nafasi ya kupata suluhu yenye ubunifu mkubwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad