HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 4, 2019

VIFO VYA MAMA NA WQTOTO KUBAKI HISTORIA CHALINZE: RIDHIWANI

Na Shushu Joel, Chalinze.
MBUNGE wa jimbo la Chalinze, wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete ameendelea na ukamiloshaji wa ahadi zake alizokuwa amewaahidi wananchi wa jimbo lake pindi alipokuwa akijinadi kuwaomba kura ili aweze kuwasaidia kuwasemea bungeni ili serikali itatue changamoto zao kwa wakati.

Maneno hayo alisema jana katika kijiji cha chahua kata ya Bwilingu jimboni humo alipokuwwa akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho.

Akizungumza na wananchi wa eneo hilo mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingI Kikwete amewapongeza wananchi hao kwa usimamizi mzuri wa fedha alizochangia katika ujenzi huo uligharimu zaidi ya milioni 40 mpaka sasa.

"Uwepo wa zahanati katika kijiji hiki utapunguza kama si kuondoa kabisa vifo vya wazazi na watoto ambavyo sio vya lazima"Alisema Kikwete.

Aliongeza kuwa wakati anawaomba wananchi hao ridhaa ya kuwa kiongozi wao aliwahakikishia kabla ya miaka 5 kumalizika atahakikisha anajenga zahanati katika kijiji hicho na hivyo jambo hilo limekamilika kwa asilimia 90. Aidha amewataka wananchi hao pindi zahanati hiyo itakapoanza kufanya kazi wapendelee kupima afya zao ili kuweza kubainika nini kinachokusumbua ili wataalamu waweze kubaini tatizo na kutatuliwa.

Hivyo mbunge huyo amewahakikishia wananchi wa jimbo hilo kuwa kila alichokiahidi atatekeleza kabla ya miaka 5 kumalika cha msingi katika mradI yote inayoletwa na serikali kwa ushawishi na ile mingine inapaswa kulindwa ili itumike kwa vizazi vingi.

Kwa upande wake Fatuma Ally mkazi wa eneo hilo amempongeza mbunge kwa jinsi anavyowapambania wananchi wa kijiji hicho katika kuhakikisha wanapata maendeleo ya kila nyanja ili kuondokana na changamoto za hapa na pale.

Aliongeza kuwa mbali na uwekaji wa jiwe la msingi katika zahanati hiyo pia umetuletea umeme,kisima kikubwa cha maji na utengenezaji wa miundombinu inayosaidia kurahisisha kwa shughuli za ufanisi wa maendeleo katika maeneo yetu.

Aidha amempongeza Kikwete kwa jinsi alivyofanikisha ujenzi wa shule ya msingi iliyokuwa to imechakaa kwa ujenzi wa madarasa matatu yenye vyumba viwili viwili hivyo hali hiyo imssaidia kuchochea kwa maudhurio mazuri ya watoto shuleni na kupata masomo yao ya kila siku.

Naye Abeid Salmu ambaye ni shehe wa msikiti wa kijiji hicho amempongeza Kikwete kwa juhudi zake za ufanisi wa kuwaletea maendeleo mbali mbali kwenye kijiji hicho bila kuchelewesha.

"Kijana wetu Ridhiwani a me kuwa akijituma sana katika uletaji wa maendeleo hivyo tunamuomba aendelee utekelezaji huo huo kwa wananchi wake"Alisema.

Aidha shehe huyo amemtoa wasiwasi mbunge huyo kuwa katika jimbo la Chalinze hakuna mbunge mwenye moyo kama wake hivyo asijitokeze mtu yeyote yule kuleta uso wake katika uchaguzi ujao kwani sie tunamjua Kikwete ndio kimbilio letu kwani muda mchache tu kafanimisha mradI mingi na mikubwa Chalinze.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad