HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 26, 2019

TIMU ZA BUNGE, WAWAKILISHI ZATOKA SARE 2-2

TIMU ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoka sare kwa kufungana mabao 2-2 na timu ya Wajumbe wa Baraza Wawakilishi katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Mtanange huo umechezwa leo (Ijumaa, Aprili 26, 2019) ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa suluhu.

Timu ya Wabunge ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata goli kwenye dakika ya pili ya kipindi cha pili   lililofungwa na Venance Mwamoto. Iliwachukua dakika mbili tu, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kusawazisha bao hilo lililofungwa na Juma Ally baada ya kupiga shuti kali la umbali wa mita 20.

Hata hivyo, goli hilo lilizua utata na kusababisha mpira huo kusimamia kwa dakika tano ili wavu wa goli urekebishwe kwa sababu mpira ulipita kwenye wavu ambao umechanika, upande wa kushoto juu ya goli.

Ilimlazimu mwamuzi Byrceson Msuya wa Dodoma awasiliane na mshika kibendera wake na hatimaye wakaridhia kuwa hilo lilikuwa ni goli.

Mara baada ya mpira kuanza, kapteni wa BLW, Hamza Hassan aliipatia timu yake bao la pili kwenye dakika ya nane baada ya kupigwa kichwa kupitia mpira wa krosi uliopigwa na Masoud Abraham.

Mpira uliendelea kwa kasi huku kila timu ikijaribu kutafuta goli ambapo kwa upande wa BLW, wachezaji Mohammed Mgaza na Juma Ali walikuwa mwiba kwa ngome ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha kwa upande wa Jamhuri ya Muungano washambuliaji Venance na Yona Kirumbi ambaye aliingia kipindi cha pili, walikuwa mwiba kwa ngome ya Baraza la Wawakilishi lakini ustadi wa golikipa wa BLW, Fakhi Suleiman ulikuwa kikwazo kikubwa kwao kwani akiokoa michomo mingi ya washambualiaji wa timu ya Bunge.

Ikiwa imebakia dakika moja mchezo huo kumalizika, mchezaji wa timu ya Bunge, Yona Kirumbi aliisawazishia timu yake bao la pili baada ya kupikea pasi ndefu kutoka kwa Onesmo Raurau.

Akitoa maoni juu ya mchezo huo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alihudhuria mechi hiyo alisema mechi ulikuwa nzuri na imetumiaka kudumisha Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar.

Pia aliahidi kwamba, kwenye maadhimishi ya mika 56 ya Muungano, timu ya Bunge itakenda kucheza uwanaja wa Aaman, Zanzibar pamoja na timu ya Baraza la Wawakilishi.

Naye Spika wa Bunge, Job Ndugai alisemw timu ya Bunge imecheza vizuri sana na ameshuhudia timu ya Baraza la wawakilishi kiwa imezidiwa, na kama wangeongeza dakika tano, ni lazima timu yale ingetoka na ushindi.

Kwa upande wake, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zuberi Ali Maulid aliwapongeza wachezaji wa timu zote mbili kwa umahiri waliounyesha na kuongeza kwamba watawasubiria mwakani timu ya Bunge Sports Club katika mtanange utakaofanyika huko Zanzibar.

Timu ya Bunge iliwakilishwa na Ally Salum, Abdallah Haji, Salum Rehani/ Pascal Haonga, Ally King/Chiza Amani, Yusuf Kaiza, Venance Mwamoto, William Ngeleja/ Yona Kirumbi, Cosato Chumi, Sixtus Mapunda/Onesmo Raurau, Godfrey Mgimwa/Peter Msigwa na Alex Gashaza/Rajab Kipilo.


Timu ya Wawakilishi ilikuwa na Fakhi Suleima, Ali Salum, Ramadhani Hamisi, Amour Mohammed, Juma Ali, Miraji Khamis, Mohammed Mgaza, Masoud Abrahman, Rashid Ali Juma/Dau Maulid, Hamza Hassan na Suleiman Sarahan.
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, wakati akiwasili katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Aprili 26, 2019, kushuhudia mpira kati ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zubeir Ali Maulid, Mbunge wa Viti maalum, Salma Kikwete.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akiwapa mkono Wabunge wa Bunge la Tanzania, wakati akikagua timu katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, katika mechi kati ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Aprili 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akiwapa mkono Wabunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakati akikagua timu katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, katika mechi kati ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Aprili 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akirusha shilingi kabla ya mechi kuanza, kati ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Aprili 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akipuliza firimbi, kwenye kati ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Aprili 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  Mbunge wa Jang’ombe Ali King, akicheza mpira wa juu, katika mechi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Aprili 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akioneshwa jambo na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zubeir Ali Maulid, kwenye kati ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Aprili 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Wabunge wakiangalia mechi kati ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Aprili 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad