HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 4, 2019

RAIS DKT MAGUFULI AENDELEA NA ZIARA YAKE YA KIKAZI MKOANI MTWARA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi wa mkoa wa Mtwara alipopita makao makuu ya mkoa ya chama hicho ili kuwasalimia akiwa njiani kuelekea kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya lami ya Mtwara-Newala na ukarabati wa Chuo cha Ualimu Kitangali kilichopo Newala Vijijini Jumatano Aprili 3, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine akikata utepe kuashiria ujenzi wa barabara ya lami ya Mtwara-Newala yenye urefu wa kilometa 50 ikiwa ni sehemu ya barabara ya Mtwara-Newala-Masasi yenye urefu wa kilometa 210 ambayo ikikamilika itapunguza urefu wa barabara ya ukanda wa maendeleo wa Mtwara kutoka kilometa 1,020 hadi kilometa 825
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia maandalizi ya kubangua korosho katika kiwanda cha Yalin Cashewnut Company Ltd kilichopo eneo la Msijute Mtwara Vijijini akiwa na Waziri wa Kilimo na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa akiwa katika ziara ya kikazi ya mkoa wa Mtwara
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua kiwanda cha kubangua korosho cha Yalin Cashewnut Company Ltd kilichopo eneo la Msijute Mtwara Vijijini akiwa na wawekezaji wa kiwanda hicho kutoka China na viongozi wazawa wa kiwanda hicho pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa akiwa katika ziara ya kikazi ya mkoa wa Mtwara 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwa la msingi kuashiria ukarabati wa majengo ya Chuo cha Ualimu Kitangali kilichopo Newala Vijijini akiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichaki, Balozi wa Canada nchini Pamela O'Donnell na viongozi wengine Jumatano Aprili 3, 2019. Mradi wa ukarabati wa chuo hicho ni moja ya miradi inayohusisha ukarabati wa vyuo vya ualimu nchini vikiwemo vya Ndala, Shinyanga na Mpuguso kwa gharama ya shilingi bilioni 36.475 ikiwa ni ufadhili wa serikali ya Canada iliyotoa shilingi bilioni 28.275 wakati serikli ya Tanzania imetoa shilingi bilioni 8.200.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Balozi wa Canada nchini Pamela O'Donnell baada ya kuweka jiwa la msingi kuashiria ukarabati wa majengo ya Chuo cha Ualimu Kitangali kilichopo Newala Vijijini akiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na viongozi wengine Jumatano Aprili 3, 2019. Mradi wa ukarabati wa chuo hicho ni moja ya miradi inayohusisha ukarabati wa vyuo vya ualimu nchini vikiwemo vya Ndala, Shinyanga na Mpuguso kwa gharama ya shilingi bilioni 36.475 ikiwa ni ufadhili wa serikali ya Canada iliyotoa shilingi bilioni 28.275 wakati serikli ya Tanzania imetoa shilingi bilioni 8.200.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako baada ya kuweka jiwa la msingi kuashiria ukarabati wa majengo ya Chuo cha Ualimu Kitangali kilichopo Newala Vijijini akiwa na Balozi wa Canada nchini Pamela O'Donnell na viongozi wengine Jumatano Aprili 3, 2019. Mradi wa ukarabati wa chuo hicho ni moja ya miradi inayohusisha ukarabati wa vyuo vya ualimu nchini vikiwemo vya Ndala, Shinyanga na Mpuguso kwa gharama ya shilingi bilioni 36.475 ikiwa ni ufadhili wa serikali ya Canada iliyotoa shilingi bilioni 28.275 wakati serikli ya Tanzania imetoa shilingi bilioni 8.200.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wana kwaya wa Chuo cha Utumishi cha Mtwara alipowasili katika kijiji cha Naliendele kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya lami ya Mtwara-Newala yenye urefu wa kilometa 50 ikiwa ni sehemu ya barabara ya Mtwara-Newala-Masasi yenye urefu wa kilometa 210 ambayo ikikamilika itapunguza urefu wa barabara ya ukanda wa maendeleo wa Mtwara kutoka kilometa 1,020 hadi kilometa 825.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Newala Mkoani Mtwara aliposimama kuwasalimia akiwa njiani kuelekea katika chuo cha Ualimu Kitangali kilichopo Wilaya ya Newala Mkoa wa Mtwara ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya siku tatu Mkoani humo. 
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwasalimia Wananchi wa Tandahimba Mkoani Mtwara mara baada ya Msafara wa Rais wa Jamhuri Dkt. John Pombe Magufuli kusimama kwaajili ya kuwasalimia alipokuwa akielekea Kuweka jiwe la msingi la ujenzi katika chuo cha Ualimu cha Kitangali Wilayani Newala Mkoa wa Mtwara. Aprili 3, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Canada Nchini Pamela O Donnell pamoja na Waziri wa Elimu  Profesa Joyce Ndalichako kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa chuo cha Kitangali kinachojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Canada Wilayani Newala Mkoa wa Mtwara. Aprili 3, 2019




Sehemu ya Majengo ya mapya ya Chuo cha Kitangali ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa chuo  hicho.


 Sehemu ya Nyumba za makazi Mapya ya Walimu wa Chuo cha Kitangali ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa chuo  hicho.
PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad