HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 7 April 2019

RAIA WA RWANDA WAISHIO NCHINI WAADHIMISHA MIAKA 25 YA MAUAJI WA KIMBARI

Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii 

RAIA wa Rwanda waishio nchini Tanzania leo Aprili 7 wameadhimisha miaka 24 ya mauaji ya kimbari yaliyopoteza zaidi ya watu milioni moja kwa siku 100 hasa kabila la Watutsi na kuacha yatima, wajane wengine wengi katika hali ngumu. Raia hao wameeleza kuwa kilichotokea hawatakisahau na hakitatokea tena. 

Akizungumza katika kumbukizi hiyo Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameeleza kuwa tukio hilo linakumbukwa pia na watanzania na kuahidi kuzidi kushirikiana nao katika masuala ya kujenga nchi na kusema kuwa hata mwaka 2016 Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli alifanya ziara nchini Rwanda alipotembelea kituo cha mauaji hayo huko Kigali na kueleza kuwa mauaji hayo yalianza kwa kupandikiza chuki katika jamii na kusisitiza kuwa hayo hayatatokea tena Rwanda na kwingineko Afrika. 
Aidha Mwakyembe ameeleza kuwa lazima tusaidiane na kushirikiana ili kuhakikisha janga kubwa kama hilo halitatokea tena. Aidha amesema kuwa mauaji hayo hayakutokea kama radi huku akiwaasa wananchi kuacha kupandikiza maneno ya chuki katika jamii. 

Kwa upande wake Balozi wa Rwanda nchini, Eugine Kayihura ameeleza kusikitishwa na tukio hilo ambalo liliathiri wananchi na taifa kwa ujumla lakini baada ya vita Rwanda iliungana tena na kuwa wamoja na kuleta maendeleo, ameeleza kuwa wanawakumbuka wenzao ambao walilengwa kuuawa na hawatasahaulika kamwe. 

Pia amesema kuwa kwa sasa wananchi wameungana pamoja na wapo sambamba katika kuleta maendeleo nchini humo. Aidha ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kudumisha mahusiano bora pamoja na jumuiya ya umoja wa mataifa kwa kuzidi kuonesha ushirikiano na wao kama taifa watazidi kusimama imara katika kuhakikisha mauaji ya aina hiyo hayatatokea tena watazidi kushirikiana, na kuwa na umoja . 
Mwakilishi wa taasisi ya kimataifa inayoshughulikia masuala yaliyosalia ya mahakama za makosa ya jinai (IRMCT) Samuel Algozin amesema kuwa miaka 25 iliyopita tangu kupotea kwa wajamii hao ambao wengi walikuwa wanawake, watoto na wazee na wengine kuachwa yatima na wajane hawatasahaulika, watakumbukwa kwa yote waliyofanya katika kulitetea taifa. 

Amesema kuwa wataendelea kulinda na kutetea haki za binadamu na kuhakikisha mauaji ya aina hiyo hayatatokea tena kama yalivyotokea mwaka 1994 na wataendelea kusimama pamoja katika kuhakikisha haki za binadamu zinatekelezwa. 

Pia Mwakilishi wa umoja wa mataifa (UN), Alvaro Rodriguez ameeleza kuwa waliouawa katika mauaji hayo nchini Rwanda miaka 25 iliyopita watakumbukwa Rwanda na kwingineko na kueleza kuwa kuokoa maisha ya watu lazima kuwe na matendo hasa kwa kuangalia masuala ya haki na usawa pamoja na kutetea haki za binadamu huku akieleza kuwa ni lazima kila nchi ijizatiti katika kutimiza malengo yake ya kulinda haki za binadamu. 

Maadhimisho hayo yalianza kwa matembezi na kufuatiwa na kwa sala fupi na baadaye mishumaa kuwashwa kama ishara ya kuwakumbuka wenzao waliouwawa kwenye mauaji hayo. Mwisho.
Balozi wa Rwanda nchini, Eugine Kayihura (wa pili kulia) akiongoza matembezi maalum ya wameadhimisha miaka 24 ya mauaji ya kimbari yaliyopoteza zaidi ya watu milioni moja kwa siku 100 hasa kabila la Watutsi na kuacha yatima, wajane wengine wengi katika hali ngumu, yaliyonyika leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiongozwa na Balozi wa Rwanda nchini, Eugine Kayihura pamoja na viongozi wengine, kuwasha mishumaa wakati wa  kuadhimisha miaka 24 ya mauaji ya kimbari yaliyopoteza zaidi ya watu milioni moja kwa siku 100 hasa kabila la Watutsi na kuacha yatima, wajane wengine wengi katika hali ngumu, yaliyonyika leo jijini Dar es salaam.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza katika maadhimisha miaka 24 ya mauaji ya kimbari yaliyopoteza zaidi ya watu milioni moja kwa siku 100 hasa kabila la Watutsi na kuacha yatima, wajane wengine wengi katika hali ngumu, yaliyonyika leo jijini Dar es salaam.
Balozi wa Rwanda nchini, Eugine Kayihura akizungumza katika maadhimisha miaka 24 ya mauaji ya kimbari yaliyopoteza zaidi ya watu milioni moja kwa siku 100 hasa kabila la Watutsi na kuacha yatima, wajane wengine wengi katika hali ngumu, yaliyonyika leo jijini Dar es salaam.


No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad