Mradi Mkubwa wa Ujenzi wa Makao ya Watoto Dodoma wenye thamani ya dola
za Kimarekani million 5.5 sawa na takriban Bilioni 10 za Kitanzania
unatarajiwa kuanza hivi karibuni katika eneo la Kikombo nje kidogo ya
Jiji la Dodoma katika eneo lenye ukubwa wa ekari 40.
Mradi huo ni wa kwanza  na wa aina yake kwa kuwa tofauti na miradi
mengine utakapokamilika utatoa huduma za utenganifu wa saikolojioa
lakini pia utatoa elimu ya ufundi kuwawezesha watoto waishio katika
mazingira magumu kupata stadi za kujitegemea na kuwezesha kaya maskini
ambazo watoto hao wanatokea ili kukabiliana na umasikini wa familia.
Mradi huo Mkubwa unajengwa kwa Msaada wa Shirika la Kimataifa la
Abbott lenye Makao yake Makuu Nchini Marekani na unajengwa Jijini
Dodoma kufuatia Serikali kuhamishia Makao Makuu ya Serikali Jijini
Dodoma hivyo kulazimika kuhamisha Makao ya Taifa ya Watoto ya
Kurasini.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile amewataka wafadhili wakubwa wa Mradi huo kutoka
Shirika la Abbott kuharakisha kuanza kwa Mradi huo mapema iwezekanavyo
na  kuhaidi kutoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha zoezi la kuanza
kwa Mradi huo.
‘’Anzeni Mradi huu kwa sasa kwa kuwa viongozi wote wako hapa Dodoma
wakishiriki katika Bunge la Bajeti hivyo kuwa rahisi kutatua mambo kwa
haraka maana mkichelewa baada ya Bunge la Bajeti watasambaa kila
mahali kutekeleza shughuli nyingine za Serikali.
Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa Mradi huu unajengwa katika Jiji ambalo
limepimwa tofauti na Makao ya Taifa ya Watoto  Kurasini ambayo kwa
sasa yako katika msongamano wa makazi ambayo hayakupimwa jambo
linalofanya Mradi huu kuwa wa aina yake hapa Nchini.
Aidha Dkt. Ndugulile ameishukuru Abbott Tanzania kwa kuanza kufadhili
Wizara ya Afya kwa upande wa Maendeleo ya Jamii kwani Shirika hilo
limekuwa Msaada mkubwa kwa upande wa Afya Tiba kwa kutoa Msaada katika
vifaa vya tiba na huduma za dharula katika hospitali.
Akitoa ufafanuzi wa Mradi huo kwa Naibu Waziri Ndugulile Kamishina wa
Ustawi wa Jamii Nchini Dkt. Naftal Ng’ondi amesema tayari Serikali ya
Mkoa wa Dodoma imetoa eneo la ekari 40 kwa ajili ya ujenzi huo na
kichosubiriwa kwa sasa ni kibali cha ujenzi wa Makao hayo mapya ya
watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
 Naibu
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. 
Faustine Ndugulile akijadiliana jambo na Makamu wa Rais wa Mfuko wa 
Abbott Tanzania Bw.Andy Wilson pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko 
huo Natalia LoBue walipofika Ofisini kwake kumpa taarifa ya Mradi wa 
Ujenzi wa Makao mapya ya Taifa ya Watoto yanayotarajiwa kujengwa hivi 
karibuni Jijini Dodoma.
 Naibu
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. 
Faustine Ndugulile akijadiliana jambo na Makamu wa Rais wa Mfuko wa 
Abbott Tanzania Bw.Andy Wilson pamoja na Kamishna wa Ustawi wa Jamii 
Nchini Dkt. Naftal Ngo’ndi wa kwanza kushoto walipofika Ofisini kwake 
kumpa taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa Makao mapya ya Taifa ya Watoto 
yanayotarajiwa kujengwa hivi karibuni Jijini Dodoma.
 Naibu
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine
 Ndugulile akijadailiana jambo na Ujumbe wa Mfuko wa Abbott Tanzania 
ulipofika Ofisini kwake kumpa taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa Makao mapya 
ya Taifa ya Watoto yanayotarajiwa kujengwa hivi karibuni Jijini Dodoma.
 Katibu
 Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu 
akijadiliana jambo na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Abbott Tanzania Bw.Andy
 Wilson alipofika Ofisini kwake pamoja na ujumbe wake kumpa taarifa ya 
Mradi wa Ujenzi wa Makao mapya ya Taifa ya Watoto yanayotarajiwa 
kujengwa hivi karibuni Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii
Dkt. Dkt. John Jingu akijadiliana jambo na Ujumbe wa Mfuko wa Abbott
Tanzania  ulipofika Ofisini kwake kumpa taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa
Makao mapya  ya Taifa ya  Watoto yanayotarajiwa kujengwa hivi karibuni
Jijini Dodoma.
 

 
 

 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment