HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 5, 2019

DEWJI AWASIHI MASHABIKI WA SIMBA KUSHANGILIA MWAZO MWISHO MECHI YA KESHO DHIDI YA TP MAZEMBE

Na Agness Francis, Blogu ya Jamii

MWENYEKITI wa klabu ya Simba Mohammed Dewji amewasihi mashabiki wa klabu hiyo kuwa  washangilie mwanzo mwisho siyo kushangilia mpaka wapate goli katika mechi inayotarajiwa kuchezwa kesho majira ya saa kumi jioni katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam ambapo klabu ya  Simba SC itaminyana na klabu ya TP Mazembe katika mchezo wa  robo Finali ya kuwania kombe la ubingwa barani Afrika. 

Dewji amezungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam  ambapo amewaomba sana mashabiki hao kuwa ikitokea bahati mbaya wamefungwa basi  waendelee kushabikia sio tu mpaka wakipata goli pia amewasihi  wabadilike kwenye hilo,  washangilie Simba  mwanzo hadi  dakika 90 za mpira zitakapomalizika. 

Hata hivyo Kufuatia mechi hiyo Mo amewawaomba mashabiki wa Simba na Watanzania kijitokeze kwa wingi uwanjani kuishangilia timu yao ili wachezaji wapate nguvu na maroli ya kufanya vizuri. 
.
"Kujitokeza kwa mashabiki kuna faida kuu mbili, moja unawaongezea nguvu wachezaji wetu na wao wanaona kuwa Watanzania wapo nyuma yao, lakini pili inawaogopesha wapinzani wetu" amesema Mo Dewji.

"Hapa hatushiriki tu, tunajiamini kwamba tunaweza na tunataka kwenda mbali zaidi ya hapa"amesema Mo. 

Ameongezea kwa kusema kuwa "Shabaha yetu sio tu kufanikiwa mwaka mmoja, tunataka kushinda kombe kila mwaka ili tushiriki Ligi ya Mabingwa kila mwaka, tunataka kushinda kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika, mimi naamini uwezo tunao, tumtangulize Mungu"amesema Dewji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad