Waziri wa Mabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipofika kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Waziri wa Mabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi wa Pili kutoka Kushoto akielezea msimamo wa Wizara yake katika kuzitangaza fursa za Uwekezaji zilizopo Zanzibar. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Muombwa.
Profesa Palamagamba Kabudi(katikati) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wa kwanza kulia akimpongeza Profesa Palamagamba Kabudi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Balozi Seif kulia na Profesa Palamagamba Kabudi
wakibadilishana mawazo mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Vuga
Mjini Zanzibar.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa
Palamagamba Kabudi alisema Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
imefanikiwa kuwa na Taifa linaloendelea kudumu muda wote kutokana na
misingi imara iliyowekwa na Waasisi wa Taifa hilo.
Alisema yapo Makabila mengi katika Mikoa na Wilaya mbali mbali Nchini
Tanzania lakini muungano wa sauti moja inayozungumnzwa na Wananchi
wake Bara na Zanzibar imekuwa mfano kwa Mataifa mengine Duniani.
Profesa Palamagamba Kabudi alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar
alipofika kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kushika wadhifa huo.
Alisema yapo Mataifa mengi Duniani yaliyowahi kuunganisha Nchi zao
akaitolea Mfano iliyokuwa Yugoslavia na sasa imesambaratika Senegal na
Gambia kwa Afrika lakini zimeshindwa kuendeleza Miungano hiyo.
Waziri Palamagamba alisema wakati Serikali zote mbili Nchini Tanzania
zinaendelea kuheshimu kwa kuweka Kumbukumbu za Waasisi hao Marehemu
Mzee Abeid Amani Karume na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,
Vizazi vya sasa vinapaswa kujifunza tabia ya Viongozi hao walioacha
msingi imara wa Umoja ndani ya Ardhi ya Tanzania.
Akigusia suala la Diploma ya Uchumi ambayo kwa sasa Tanzania
imeelezekeza nguvu zake kupitia Balozi zake zilizoko nje ya mipaka ya
Nchi Profesa Palamagamba alisema Serikali inaendeleza mfumo wa
kushawishi Wawekezaji ili kuunga mkono jitihada za Taifa za kuwa na
Tanzania ya Viwanda ifikapo Mwaka 2025.
Alieleza kwamba jitihada zinafanywa za kutangaza uimarishaji wa fursa
za Kiuchumi zinazopatikana kutokana na rasilami nyingi zilizopo Nchini
ambazo uwekezaji wake unaweza kusaidia soko la ajira na mapato ya
Taifa.
Alielezea umuhimu wa mkakati wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa
Kuimarisha Uchumi wake unaopaswa kuendelea kuungwa mkono Serikali ya
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika muelekeo wa kuelekea kwenye
Maendeleo ya haraka.
Akigusia Sekta ya Utalii inyoonekana Zanzibar kufanya vyema, Waziri
Palamagamba alisema Sekta hii muhimu hivi sasa kwa mapato ya Taifa
lazima iwekewe utaratibu wa pamoja utakaosaidia kuuza haiba ya pande
zote mbili za Muungano.
Alisema vipo vivitio vinavyopaswa kutangazwa kwa pamoja Bara na
Zanzibar ambavyo vinaweza kutoa nguvu ya ushawishi wa Watalii kufanya
ziara ya makusudi ya kutembelea sehemu zote mbili kwa wakati mmoja.
Waziri huyo wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
alielezea faraja yake kutokana na Zanzibar kupiga hata kubwa katika
kuimarisha Sekta ya Utalii inayoonekana kutoa ajhira kubwa hasa kwa
kundi kubwa la Vijana.
Alifahamisha kwamba ongezeko kubwa la idadi ya Watalii wanaotembelea
Zanzibar inayopanda kila kukicha imethibitisha uwepo wa mafanikio
katika kuendeleza Sekta hiyo muhimu.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi alisema ushawishi wa Uwekezaji ndani ya Visiwa vya Zanzibar
unapaswa kuungwa mkono na Ofisi zote za Kibalozi za Tanzania zilizopo
Mataifa mbali mbali Duniani.
Alisema Zanzibar ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo
ushawishi wake kwa Wawekezaji na Mataifa ya kigeni unawajibika
kusimamiwa na Mabalozi wa Tanzania kupitia Wizara yake ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Balozi Seif alimueleza Profesa Palamagamba kwamba Zanzibar kupitia
Viongozi wake wote waliopita na waliopo hivi sasa bado wanaendeleza
sera na Mikakati iliyoacha na Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar
Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
Alisema uimarishaji wa Miundombinu ya Mawasiliano, Ujenzi wa Nyumba za
Kisasa za Maendeleo, Afya, Elimu pamoja na huduma za Maji safi na
salama ni miongoni mwa Sekta zinazoendelea kuimarishwa na Viongozi
wote.
Balozi Seif Miradi iliyobuniwa na Serikali ya Mapinduzi ya ujenzi wa
Miji Mipya kama ule wa Ng’ambo tuitakayo katika eneo la Kwahani na
Mtaa wa Chumbuni imelenga kustawisha maisha ya Wananchi wake ili
kuachana na matumizi mabaya ya Ardhi ndogo iliyopo.
No comments:
Post a Comment