HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 2 April 2019

BABA ADAIWA KUMNYONGA MWANAE HADI KUFARIKI DUNIA, AKIDAI SIO MTOTO WAKE

Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha 

JESHI la polisi mkoani Pwani linamshikilia Robison Enerst (33) fundi ujenzi kwa tuhuma ya kumnyonga shingo,  mwanae Modesta Robison mwezi umri wa miezi sita, akidai sio mtoto wake. 

Kamanda wa polisi mkoani hapo, ACP Wankyo Nyigesa, alieleza kwamba, tukio hilo limetokea April mosi, mwaka huu  huko mtaa wa Vitendo kata ya Misugusugu ,Kibaha. 

"Kabla ya kuolewa na mtuhumiwa, mama wa mtoto (marehemu)  alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine ambae mtuhumiwa anamtuhumu ndio baba halali wa mtoto " "Hali hiyo ilisababisha migogoro ya mara kwa mara kati ya wazazi hao "alifafanua Wankyo. 

Wankyo alibainisha, wamemkamata mtuhumiwa ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria na mwili wa marehemu umehifadhiwa hospital ya rufaa ya mkoa ya Tumbi, kabla ya kukabidhiwa ndugu kwa mazishi. 

Kamanda huyo alitoa rai kwa wananchi, kuwa wanapokuwa na mashaka na jambo fulani la kihalifu watoe taarifa mapema katika vituo vya polisi ili yaweze kushughulikiwa mara moja kabla ya kuleta madhara yeyote kwa lengo la kudhibiti watuhumiwa. 

Hata hivyo, baada ya kumhoji mama wa marehemu yeye alidai mtuhumiwa alishafanya majaribio ya mtuhumiwa kumuua marehemu mwanae mara mbili.  Anaeleza, mara ya kwanza alitaka kumpa sumu ya vidonge lakini mama huyo aliwahi kumuokoa .

"Mara ya pili mtuhumiwa alinoa panga ili amkate mtoto lakini hakufanikiwa pia kufikia april 1, ambapo alimuua mtoto kwa kumnyonga shingo hadi kufariki dunia "

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad