ZOEZI LA UPIMAJI WA MARADHI YA MOYO LAANZA MKOANI ARUSHA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 11 March 2019

ZOEZI LA UPIMAJI WA MARADHI YA MOYO LAANZA MKOANI ARUSHA

Na Vero Ignatus, Arusha
Imeelezwa kuwa 75%ya vifo vinavyotokea katika mataifa yanayoendelea ukanda wa Afrika ikiwemo Tanzania vinasababishwa na magonjwa yasiyoambukizwa kwa utafiti uliofanywa 2012 na shirika WHO.
Hayo yamesemwa na Dkt Bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya inayojihusisha na magonjwa ya moyo ya JKCIA Dkt Samwel Rweyemamu katika Uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maradhi ya moyo mkoani Arusha.

Amesema kuwa kutokana na takwimu zilizofanywa 2016 wilayani simanjiro mkoa wa Manyara zinaonyesha kuwa 30%ya wanaume wote waligundulika kuwa na shinikizo la damu, hiyo ikiwa ni data zinazofanana za watu wanaoishi mjini.
 
'' Data zinaonyesha tukiweza kupambana shinikizo la damu, uzito uliokithiri, kuangalia sukari kwenye miili yetu na kupima mafuta kwenye mwili tutapunguza vifo kwa 80% '' alisema Dkt Rweyemamu

Kwa upande wa mwenyekiti wa Bodi Balozi Dkt. Ladis Komba amesema kuwa azma la AICC katika eneo la Afya lina shabiana na azma ya serikali katika kusogeza huduma bora kwa wananchi wengi zaidi

Amesema AICC itaendelea kuwa mstari wa mbele kwenye kutoa huduma za Afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na huduma ya upimaji ili kufanikisha malengo ya hospitahi hiyo na kwa Taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi wa AICC Elishilia Kaaya amesema kuwa kwa mujibu wa wataalam wa Afya magonjwa haya yanatokana na kubadilika kwa mtindo wa maisha ambapo watu wengi hawapati muda wa kufanya mazoezi kutokana na kuelemewa na ratiba za kazi za ofisini na kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya magonjwa haya.
 
' 'Magonjwa haya kwa bahati mbaya hayaonyeshi dalili za wazi na hivyo ni vigumu kwa mtu anayeugua maradhi haya kujitambua mapema hivyo kuchelewa kupata matibabu, na mara nyingi imepelekea watu wengi kupoteza maisha ghafla na wengine kupata ulemavu wa kudumu' 'alisema

Zoezi hilo la upimaji wa Afya ya moyo linatarajia kuchukua wiki moja kuanzia tarehe 11-18 marchi, hivyo wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kupima afya ya moyo pamoja na shinikizo la damu.

Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo Samwel Rweyemam kutoka JKCI akimpima Mwenyekiti wa Bodi AICC Dkt. Ladis Komba leo Jijini Arusha katika uzinduzi wa upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza.

Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo Samwel Rweyemam kutoka JKCI akimpima Kaimu mkurugenzi wa AICC Mkunde Senyagwa Mushi leo Jijini Arusha katika uzinduzi wa upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kuja kupima afya zao leo katika uzinduzi wa upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad