HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 27, 2019

WAZIRI MKUU AIPONGEZA OFISI YA RAIS - UTUMISHI KWA KUKAMILISHA UJENZI WA OFISI YAKE KWA WAKATI KWENYE MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) amewapongeza viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa usimamizi mzuri uliopelekea kumalizika kwa ujenzi wa ofisi hiyo  kwa wakati iliyopo mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Pongezi hizo amezitoa mapema  leo, alipotembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo kwenye mji wa serikali, eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Mhe. Majaliwa amesema kuwa, ameridhishwa na kiwango cha ujenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iliyojengwa ndani ya kipindi cha miezi mitatu na kwa gharama nafuu ya kiasi cha shilingi bilioni moja iliyotengwa na serikali.
 “Serikali imekuwa ikifuatilia hatua zote za ujenzi katika mji wa serikali ili kuhakikisha ujenzi unafanywa kwa viwango, na jengo la Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora limekuwa likienda vizuri sana katika hatua zote” amesema Mhe. Majaliwa.
Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa, anatambua kwamba Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora imeshafanya uzinduzi wa jengo lake, jambo ambalo ni jema na limeonyesha namna ambavyo ofisi hiyo imetekeleza vema maelekezo ya serikali.
Aidha, Mhe. Majaliwa ameweka bayana kuwa, uzinduzi rasmi wa Ofisi zote zilizojengwa kwenye mji wa serikali utafanywa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika tarehe rasmi atakayoipanga.
Mhe. Majaliwa ametoa wito kwa ofisi hiyo kuboresha mandhari ya nje ya  ofisi ili iweze kupewa kipaumbele na serikali kuwa ofisi itakayotumika kwa ajili ya  uzinduzi wa ofisi zote  zilizojengwa kwenye mji huo wa serikali. 
Naye, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amemshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) kwa kutenga muda wake kuitembelea Ofisi ya Rais - Utumishi na Utawala Bora katika mji wa serikali, na kumshukuru kwa namna alivyowahimiza mawaziri kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa ofisi zao kwenye mji wa serikali ili ukamilike kwa wakati.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, amemuahidi Mhe. Majaliwa kuwa, ofisi yake itatekeleza maelekezo aliyoyatoa na itaendelea kutekeleza maagizo anayoyatoa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Awali, Kaimu Meneja wa Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Bw. Herman Tanguye amesema kuwa, Wakala ya Majengo Tanzania imekamilisha ujenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa asilimia 99.5% kwa muda uliopangwa na kwamba hatua iliyobakia ni kukamilisha mandhari ya nje ya ofisi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa ameitembelea Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi za serikali kwenye mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma, kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuzindua ofisi hizo rasmi hivi karibuni.
 Muonekano wa jengo jipya  la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) na ujumbe wake wakiwasili katika jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo kwenye mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) akiwa ndani ya ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) iliyopo kwenye mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma. Kulia kwake ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) akizungumza  na baadhi ya viongozi na watumishi wa umma kwenye mji wa serikali, mara baada ya kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  lililopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) akifurahia jambo mara baada ya kuzungumza na baadhi ya viongozi na watumishi wa umma kwenye mji wa serikali, mara baada ya kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  lililopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akitoa neno la shukrani kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb), mara baada ya Mhe. Majaliwa kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  lililopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael wakifurahia jambo na viongozi wengine mara baada ya kukamilika kwa ziara ya Mhe. Kassim M. Majaliwa ya kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo kwenye mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad