WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa
Tanzania nchini Zambia, Mheshimiwa Balozi Hassan Simba Yahya, ambapo
amemtaka akaimarishe mahusiano baina ya nchi zote mbili.
Amekutana
na Balozi Yahya leo (Jumamosi, Machi 23, 2019) katika Ofisi ya Waziri
Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu pamoja na mambo mengine
amemtaka balozi huyo kuhakikisha anaboresha shughuli za Kidiplomasia
kati ya Tanzania na Zambia.
Pia,
Waziri Mkuu amemtaka akakutane na wafanyabiasha wa Zambia na
awahamasishe waje wawekeze katika sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda.
Amesema Balozi huyo anaweza kuandaa kongamano la biashara na uwekezaji
kwa kuwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Zambia
ili kuboresha uchumi.
Kwa
upande wake, Balozi Yahya amesema atahakikisha anayafanyia kazi
maelekezo yote aliyopewa ikiwa ni pamoja na kuimarisha biashara pamoja
na kuboresha ushirikiano baina ya Tanzania na Zambia.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini
Italia waje wawekeze nchini na Serikali itawapa ushirikiano wa kutosha.
Ameyasema hayo leo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia
nchini, Balozi Roberto Mengoni.
Akizungumza
na Balozi huyo Ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni, Dar es salam, Waziri
Mkuu amesema Tanzania ipo tayari kuwapokea wawekezaji kutoka kwenye nchi
hiyo. “Serikali imedhamiria kuendeleza sekta ya viwanda nchini ili
kukuza uchumi na kufikia wa kati ifikapo 2025, hivyo tunawakaribisha
wafanyabiashara waje wawekeze”.
Amesema
Tanzania iko tayari wakati wote kutoa ushirikiano ili kuhakikisha
wawekezaji watakaojitokeza kuwekeza nchini wanafanikiwa ili mataifa yote
yaweze kufaidika, ambapo Ofisi yake kupitia Waziri mwenye dhamana ya
Uwekezaji, Bibi Angela Kairuki yuko tayari kuwasikiliza na kuwasaidia
wawekezaji wote wanaokusudia kuwekeza nchini.
Naye,
Balozi Mengoniameishukuru Serikali kwa ushirikiano mzuri uliopo baina
ya Tanzania na Italia, hivyo amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba
watauendeleza na amesema wapo tayari kushirikiana na Tanzania
kuhakikisha mkakati wa Serikali wa kukuza uchumi kupitia sekta ya
viwanda unafanikiwa.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Zambia,
Mhe. Hassan Simba Yahya kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri
Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Machi 23, 2019.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini
Zambia, Mhe. Hassan Simba Yahya ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni
jijini Dar es salaam, Machi 23, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Italia Nchini, Mhe.
Roberto Mengoni, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam,
Machi 23, 2019.
No comments:
Post a Comment