HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 11, 2019

Wanawake waaswa kujituma ili kuleta maendeleo

Wanawake nchi wameaswa kuendelea kufanya kazi kwa bidii pamoja na kujituma ili kuleta maendeleo kwa ajili ya familia zao na taifa kwa ujumla licha ya changamoto ambazo wanakubana nazo.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tanzania Saccos for Women Enterpreneurs (Taswe – SACCOS) Anna Matinde wakati akiongea na wanawake wanafanyi kazi wa Airtel Tanzania wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo yaliandaliwa na kampuni hiyo.

Imekuwa ni kawaida kwa wanawake kulalamika kwamba hawapewi fursa sawa na wanaume ili kuonyesha uwezo wao. Na hii ni popote unapoenda. Wanawake wanasema wanaume ndio wenye furs azote na wao wamekuwa ni kama kivuli kwao. Mimi nataka kuwaambia huo sio ukweli. Sisi wanawake tunao nguvu na fursa kwa wanaume ya kuweza kufanya hata Zaidi yao. Tunachotakiwa kufanya ni kujiamini na kufanya kazi kwa bidii ili kujijengea heshima kwenye jamii yetu, alisema Matinde.

Matinde alisema kauli mbiu ya siku ya wanawake duniani mwaka huu ni #BalanceforBetter’ ikimaanisha kwamba kuwaza kwa mbali na kujiandaa kwa mafanikio. Ni muhimu kutambua kwamba wanawake tunaitaji kujikwamua kiuchumu na kuwa na uhuru wa kifedha. Vile vile tunatakiwa kufanya kazi kwa bidii, nyumbani na sehemu zetu za kazi. Lakini muhimu tunatakiwa kuwa wajasiriamali. Hatuwezi kuendelea kuishi kwa kutengemea mishahara yetu au waume zetu. Ni muhimu kuangalia namna ya kujibadilisha fikra zetu kwenye ujasiriamali ili kuwa na uhuru wa kiuchumi, alisema Matinde.

Mimi nina uzoefu wa kutosha wa kuajiriwa na pia wa ujasiriamali. Wakati naanza maisha ya ujasiriamali hakuna mtu yeyote aliyekuwa anafikiria kama naweza kuwa hapa nilipo leo. Nawaomba mtumie kila dakika yenu kufanya kitu ambacho kitaweza kuwaingizia kipato cha ziada. Ni lazima muelewe ya kwamba wanawake wanayo nguvu ya kupata chochote unachohitaji kama tu mtakuwa na malengo, kufanya kazi kwa bidii na kuwa na mawazo chanya, aliongeza Matinde.

Akiongea kwenye maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano aliwaaza wanawake kujishusha na kuendeleo kufanya kazi kwa moyo wote na bidii ili kuleta mafanikio.

Natoa wito kwa wanawake wote kutokata tamaa. Tunaweza kupata changamoto za hapa na pale lakini cha muhimu ni kujitambua na kuendelea kung’aa. Ni lazima muwe na mawazo chanya lakini muhimu Zaidi ni kuendelea kumuomba Mungu atuongoze na kila jamba, Singano alisema.

Hii ni siku ya wanawake na kusherekea ni kitu cha muhimu. Lakini ni lazima kutafakari na kujiweka juu zaidi. Sisi ni watu muhimu kwenye jamii na ni vizuri kuelewa tunayo fursa za kimaisha sawa na wanaume. Tufanye kazi kwa bidii, tujiheshimu na tutumie muda wetu vizuri ili tufanikiwe, aliongeza Singano.
 Mkurugenzi wa Kitengo cha Rasimali Watu Airtel Tanzania Stella Kibacha akitoa mada wakati wa mkutano wa wafanyakazi wa Airtel Tanzania uliandaliwa na kampuni ikiwa na maadhimisho ya kusherehekea siku ya wanawake duniani ambayo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Wafanyakazi wanawake Airtel Tanzania wakionyesha ujuzi wao wa kucheza muziki wakati wa mkutano wa wafanyakazi wa Airtel Tanzania uliandaliwa na kampuni ikiwa na maadhimisho ya kusherehekea siku ya wanawake duniani ambayo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
Kutoka kulia Mkurugenzi na Mwanzilishi wa taasisi ya Tanzania Saccos for Women Entrepreneurs (Taswe-Saccos) Anna Matinde, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice na Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo Adriana Lyamba kwa pamoja wakikata keki wakati wa mkutano wa wafanyakazi wa Airtel Tanzania uliandaliwa na kampuni ikiwa na maadhimisho ya kusherehekea siku ya wanawake duniani ambayo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad