HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 10, 2019

UMMY MWALIMU AKEMEA WAAJIRI SEKTA BINAFSI KUFUKUZA KAZI WANAWAKE WAJAWAZITO


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu ( wa pili kulia) akiangalia bidhaa zinazozalishwa na wanawake wa Mkoa Mwanza katika moja ya banda lililokuwepo katika viwanja vya Kisesa Bujora wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani humo kulia ni Mwalikishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake UN Women Bi. Hodan Addou na wa tatu kulia ni Balozi wa Sweden Bw. Anders.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametaka kupewa taarifa za waajiri wote hasa Sekta Binafsi waliowafukuza wanawake kazi au kuwashusha vyeo kwa sababu wamepata ujauzito wakiwa kazini.

Ameyasema hayo mkoani Mwanza alipokuwa akizungumza na Wanawake na wananchi wa Mkoa wa Mwanza katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Aidha ameitaka Jamii katika maeneo ya kazi kuondokana na rushwa za ngono jambo ambalo ni tatizo katika upatikanaji wa haki za wanawake na waajiri wa Sekta za Binafsi kuzingatia utu na haki za wanawake wafanyakazi.

“Mwanamke kupata mimba ni haki yake ya asili kutokana na uumbaji wa Mungu na hivyo ni marufuku kuwafukuza kazi Wanawake wafanyakazi hasa Sekta Binafsi kisa kuwa na ujauzito” alisema.

Ameongeza kuwa suala la usawa wa kijinsia ni muhimu kwa wanaume kushiriki kwani wao ni pia ni wahusika wakuu wa kuwepo kwa vitendo vya Ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Waziri Ummy amesema yeye kama Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Wanawake atahakikisha wanapata fursa sawa katika masuala muhimu kwa manufaa ya haki na ustawi wao.

Ameagiza kutekelezwa kwa haki ya Mwanamke kunyonyesha mara baada ya kumaliza likizo zao za uzazi kwani ni suala la muhimu sana kwa Mtoto kupata maziwa ya mama katika ukuaji wa Mtoto katika umri wa miezi ya awali.

Aidha Waziri Ummy amekemea vitendo vya rushwa ya nono na kuipongeza Taasisi ya kuoambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU
kwa kukiona suala hilo ni moja kti ya vitendo vya kikatili afanyiwavyo mwanamke na kumyima haki yake.

Akimkaribisha mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Philis Nyimbi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana amesema mkoa unatekeleza mikakati mbalimbali katika kumuwezesha Mwanamke na Mtoto wa kike kwa kumuweka mbali na Vitendo vya Ukatili dhidi yao ili kuwawezesha kupata fursa zitakazowezesha kufikia usawa wa kijinsia.

Naye Mwakilishi Mkazi Umoja wa Mataifa Bw. Alvaro Rodriguez amesema kuwa Umoja wa Mataifa unataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa kuhakikisha kunakuwepo na usawa wa kijinsia na kuondoa vikwazo vyote vinavyosababisha kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia kama vile mimba na ndoa za utotoni ambazo zimekuwa zikiwanyima fursa watoto wa kike kutimiza ndoto zao.

Ameongeza kuwa mapambano wa usawa wa kijinsia yatafanikiwa pale yatakaposhirikisha wanaume na wavulana katika kuhakikisha wasichana na Wanawake wanapata fursa sawa katika kutimiza ndoto zao.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake UN Women Bi. Hodan Addou amesema kuwa Shirika hilo linashirikiana na Serikali na Mashirika ya kitaifa kuhakikisha elimu inatolewa na usawa wa kijinsia inakuwa suala la kipaumbele katika Jamii zetu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad