HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 20 March 2019

Tumewekeza nguvu katika huduma ya afya ya uzazi ya Mama na Mtoto-Dkt.Ndugulile

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Serikali imesema kuwa imewekeza katika huduma za  Afya ya Mama na Mtoto katika kuhakikisha wanawake  wa wote wanajifungua katika sehemu salama.

Hayo ameyasema Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipokutana na Mtandao wa Utepe Mweupe Kitaifa wenye kampeni ya Mwanamke anataka Nini, Ndugulile amesema kuwa hali ya upatikanaji wa huduma za afya nchini zimeboreshwa ikiwemo huduma ya uzazi kwa kujenga vituo vya afya 350 ambapo huduma za uzazi zinatolewa.
Amesema kuwa tatizo la wanawake kujifungulia koridoni katika vituo vya zimepungua na mwisho wa siku zitaisha kabisa kutokana na jitihada za serikali zinazofanywa.

Amesema kuwa serikali imeajiri wafanyakazi 11000 wa sekta ya afya ili kuweza kutoa huduma zenye ufanisi  katika Hospitali na vituo vya afya nchini. Dkt.Ndugulile amesema  kuwa katika katika uwekezaji huo wameboresha Hospitali 67 nchini kwa kuwa na huduma zote kwa kuzingatia huduma za uzazi ya Mama na mtoto.

Amesema kuwa vifo vya wa Mama na Watoto wanategeemea katika twakimu zijazo zitakuwa zimepungua kutokana na uwekezaji uliofanywa katika sekta ya afya. Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mtandao wa Utepe Mweupe Kitaifa Rose Mlay amesema kuwa katika kampeni hiyo mwanamke anataka Nini baada ya kuwahoji wanawake wamekuwa wakitaka huduma ziboreshwe katika huduma ya uzazi huku wakitaka zitolewe bure pamoja na vifaa mbalimbali.

Mlay amesema kuwa katika mahojiano baadhi wanataka serikali iongeze vituo vya afya vya kufanya kila mwanamke aweze kufikia.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na Mitandao wa Kuratibu wa Utepe Mweupe katika ofisi Wizara ndogo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Utepe Mweupe Kitaifa Rose Mlay akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile kuhusiana na Kampeni ya wanataka nini inayoratibiwa na mtandao huo.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad