HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 8, 2019

StarTimes yatoa msaada kwa kituo cha watoto CHAKUWAMA

 Siku ya kimataifa ya wanawake duniani husherehekewa kila mwaka inapofika tarehe 8 ya mwezi Machi. Katika kuadhimisha siku hiyo, wafanyakazi wanawake kutoka Kampuni ya Star Media (T) Ltd walitembelea kituo kinacholea watoto wenye uhitaji cha CHAKUWAMA na kukabidhi msaada kwa ajili ya matumizi mbalimbali kituoni hapo.
Miongoni mwa vitu vilivyotolewa na StarTimes ni magodoro ya kulalia, mitungi ya gesi, pampers kwa ajili ya watoto wadogo, mchele, maharage, unga wa mahindi, maziwa ya unga, maji ya kunywa, sharubati, sukari, mafuta ya kupikia, nyanya na vitunguu pamoja na pesa taslim Tsh 450,000 kwa ajili ya kulipia umeme na maji.

“Katika siku hii muhimu ya kuadhimisha wanawake duniani, tuliona ni vyema kushiriki na wenye mahitaji kwa kila tulichojaaliwa tunarudisha kwa jamii hii inayotuzunguka. Tunaamini katika kutoa kwa sababu ndipo ubinadamu ulipo. Tumefarijika sana kuwaona mkiwa na furaha.” Joan Usiri Afisa Rasilimali watu, StarTimes.
Kituo cha CHAKUWAMA kipo jijini Dar es Salaam mtaa wa Sinza na kwa sasa kina jumla ya watoto 68 wenye umri kati ya mwaka mmoja hadi ishirini.
“Tunawashukuru sana kwa msaada huu mliotuletea lakini zaidi kwa upendo wenu na kukumbuka kuwa kuna jamii ambayo ingeweza kufaidika na mchango wenu. Mungu awabariki sana. Sisi tutaendelea kuwalea katika maadili mema ili badae waje kuwa kama nyinyi na pengine wasaidie watu wengi zaidi.” Bw. Hassan Katibu wa kituo cha CHAKUWAMA.
 Afisa Rasilimali watu Kampuni ya StarTimes, Joan Usiri (kulia) akikabidhi msaada kwa Katibu wa kituo cha CHAKUWAMA  Hassan

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad