HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 14, 2019

RC HAPI AZINDUA JUKWAA LA NAWEZA MKOANI IRINGA

MKUU wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi leo amezindua Jukwaa litakaloshughulikia maswala ya Afya kwa Watu wazima hususani Afya ya Mama na Mtoto Mkoani Iringa.

NAWEZA ni Jukwaa linalolenga kufikisha elimu sahihi itakayowajengea uwezo wananchi wabadili tabia na mitizamo hasi ili kuleta matokeo chanya ya kiafya. Akizindua jukwaa hilo Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ali Hapi alisema lengo la serikali ni kupunguza vifo vya uzazi na watoto wachanga vinavyosababishwa na changamoto mbalimbali zikiwemo huduma duni  na ukosefu wa elimu  na matumizi sahihi ya huduma za afya na afya ya uzazi.

Alisema kuwa serikali kwa kushirikiana na mradi wa USAID Tulonge Afya fhi 360 inajitahidi kuelimisha jamii juu ya afya ya uzazi katika kupunguza vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua, vifo vya watoto wachanga lakini pia vifo vinavyotokana na ugonjwa wa malaria.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa vyombo vya habari vina jukumu kubwa la kuisaidia serikali kwa kufikisha ujumbe na elimu sahihi kwa wananchi na jamii  wapate uelewa na umuhimu wa kuwa na afya bora itakayowawezesha kushiriki shughuli za uzalishaji na kuinua uchumi wao.

Kwa mujibu wa Hapi jukwaa hilo litatoa huduma jumuishi za afya katika maeneo ya afya ili kuiwezesha serikali kufanikisha mikakati na vipaumbele vyake vya kupunguza maambukizi ya Ukimwi (VVU), vifo vya  akina mama vitokanavyo na uzazi,vifo vya watoto wachanga, malaria na kifua kikuu (TB).
Aidha, alisema kukosekana kwa taarifa  sahihi za masuala ya afya kumesababisha wananchi wengi wakose elimu sahihi  ya matumizi ya afya ya uzazi na hivyo kushindwa kubadili tabia zao kiafya.

"Takwimu zinaonyesha kuwa vifo vya akina mama  556  hupoteza maisha kila mwaka  kati ya vizazi hai 100,000  huku watoto wakiwa  25 kati ya 1,000  nao wakifariki baada ya kuzaliwa, hivyo serikali inataka hali ibadilike  ifikapo 2020,"alisema Hapi na kuongeza kuwa nia ya serikali ni kuonavifo vya wajawazito vinapungua hadi kufikia 292  na watoto chini ya miaka 5 vishuke  na kufikia 16 kwa mwaka.

Hata hivyo asilimia  25 ya kina mama ndio wanaokwenda kliniki baada ya kupata ujauzito, huku 63 asilimia wakijifungulia vituo vya afya hivyo NAWEZA inalenga kuwasaidia katika changamoto za maradhi na ujauzito.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi  akizungumza na wadau wa Afya wa Mkoa wa Iringa (hawapo pichani) mara baada ya kuzindua Jukwaa la “NAWEZA” litakalozungumzia maswala ya Afya kwa watu wazima hususani Afya ya Mama na Mtoto.Uzinduzi huo umefanyika leo Mkoanim humo.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi (kushoto) na Mwakilishi kutoka USAID, Ananthy Thambinayagamwa wakipiga makofi mara baada ya Mkuu wa Mkoa kuzindua Jukwaa la “NAWEZA” litakalozungumzi maswala ya Afya kwa watu wazima hususani Afya ya Mama na Mtoto.Uzinduzi huo umefanyika leo Mkoanim humo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali mara baada ya kuzindua Jukwaa la “NAWEZA” litakalozungumzi maswala ya Afya kwa watu wazima hususani Afya ya Mama na Mtoto.Kulia ni Mwakilishi kutoka USAID Tulonge Afya, Jacqueline Larsen, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela na Mwakilishi kutoka USAID, Ananthy Thambiayagam.Uzinduzi huo umefanyika leo Mkoani humo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad