HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 29, 2019

NMB YAWAHAKIKISHIA WAKAZI WA LINDI KUWAPA HUDUMA BORA NA KWA WAKATI


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk harrison Mwakyembe akisikiliza maelezo ya Meneja NMB kanda ya Kusini Janeth Shango alipotembelea banda la benki hiyo kabla ya ufunguzi wa Jukwaa la tisa la fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani Lindi.

Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Kilimo wa benki ya NMB, Carol Nyangaro akitoa mada baada ya ufunguzi wa Jukwaa la tisa la fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani Lindi.

……………..

BENKI ya NMB imewahakikishia wajasiriamali, wafanyabiashara na wakulima mkoani Lindi kuwa itaendelea kuwahudumia kupitia huduma zake za kutunza fedha lakini pia kwa utoaji wa mikopo.

Hayo yalibainishwa na Meneja wa Kanda ya Kusini wa benki hiyo – Janeth Shango, wakati akizungumza kwenye jukwaa la fursa za biashara na uwekezaji lilofanyika mkoani humo. Kama wadau wa sekta ya biashara nchini, Benki ya NMB imedhamini wa jukwaa la Biashara linalofanyika mkoani Lindi.

Jukwaa hilo lililoandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, liliwakutanisha washiriki takribani 350 wakiwemo wawekezaji, wakulima, wajasiriamali, wafanyabiashara, taasisi mbalimbali na viongozi mbalimbali wa serikali.

Benki hiyo imefanya vizuri katika sekta ya kilimo na kwa kutoa mikopo kulingana na mnyororo mzima wa zao husika kupitia matawi yake 7, pamoja na kutoa huduma zingine za kifedha kupitia mawakala zaidi ya 105 na mashine za kutolea fedha za ATM mkoani humo.

Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Kilimo wa benki hiyo Carol Nyangaro alisema katika benki hiyo ambayo serikali ina hisa ya asilimia 30 kupitia bodi ya mikopo iliidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 500 kwa ajili ya mikopo ya wakulima na tayari shilingi bilioni 450 zimetumika.

NMB ni benki inayotambua kuwa kilimo ndio uti wa mgongo nchini kwani asilimia 75 ya watanzania wanajishughulisha na kilimo na hivyo itaendelea kuwekeza zaidi katika kilimo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad