HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 4, 2019

Mkandarasi wa REA Mkoani Rukwa kukataliwa kuendelea na mradi

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amesisitiza kukataliwa kuendelea na utekelezaji Mradi wa Mmeme Vijiji (REA) mkandarasi Nakuroi Investment kwa kushindwa kufikia hata nusu ya utekelezaji wa mradi huo hadi kufikia mwezi Februari mwaka huu.

Mkandarasi huyo ambaye alitegemewa kutekeleza mradi huo katika vijiji 111 vya mkoa wa Rukwa tangu mwezi Novemba mwaka 2017 aliposaini mkataba na kumalizika mwezi June mwaka 2019 huku akiwa amekamilisha mradi katika vijiji 23 tu hadi kufikia februari mwaka 2019.

“itakapofika mwezi June huenda hata robo tutakuwa hatujafika, kwa hali hii niseme tu wazi huyu Mkandarasi Nakuroi Investment mimi naona uwezo wake ni mdogo lakini pia eneo amepewa ni kubwa sana huyu anashughulikia Mkoa mzima vijiji tulivyonavyo ni 339 mkoani kwetu, hap ani lazima wizara ifanye kitu, mi niseme tu wazi kuwa ikifika mwisho wa mkataba wake hatutamkubali tena kuendelea na mkataba mwingine, watuongezee wakandarasi, tunahitaji kupata umeme katika vijiji vyetu vyote kwa mujibu wa mkataba,” Mh. Wangabo Alisisitiza.

Kauli hiyo imetoka wakati wa majadiliano juu ya kusuasua kwa utekelezaji wa mradi REA katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichowashirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo katika mkoa ambapo hoja hiyo iliwasilishwa kutoka katika maazimio ya kikao cha kamati ya ushari ya Wilaya ya Sumbawanga iliyowasilishwa katika kikao hicho.

Kwa upande wake Kaimu meneja wa TANESCO Mkoani Rukwa Gilles Daniel alikiri kusuasua kwa utekelezaji wa mradi huo huku akieleza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ili kuhakikisha maagizo ya serikali yanatekelezwa kwa wakati na wananchi wote wanapata umeme ambao serikali imewaahidi.

Alisema kuwa changamoto kubwa imekuwa ni upatikanaji wa vifaa kwaajili ya mradi jambo lililosababishwa na uzalishaji mdogo wa vifaa hivyo kwenye viwanda vya ndani na pia kukosa ubora unaotarajiwa.

“umeme umewashwa katika vijiji 23 tu peke yake, ni kweli kwamba mradi unasuasua hatujaenda kwa kasi ile ambayo inatakiwa kwasababu ya changamoto nyingi ambazo zimetokea zinazosababisha mradi kusuasua lakini ni juzi tu waziri alitoa maagizo ya kuwashwa vijiji vitatu kwa kila Wilaya na utekelezaji umeanza na ndani ya siku mbili umeme utakuwa yumewashwa ndani ya vijiji vitatu kila wilaya,” alisema.

Akitetea hoja hiyo Mbunge wa Sumbawanga Mjini Mh. Aeshi Hilaly amesema kuwa si vyema kuwatwisha mzigo huo Shirika la Umeme na hivyo ni jukumu la waheshimiwa wabunge wa mkoa wa Rukwa kwa ushirikiano kulichukua hilo na kulifikisha bungeni ili kulipatia ufumbuzi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad